-
Mfalme wa Saudia akumbwa na matatizo ya kiakili, haruhusiwi kuona wageni
Jun 01, 2016 23:03Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia amekumbwa na maradhi mabaya mno ya kiakili kiasi kwamba wageni wanazuiwa kumtembelea. Mwanae Mfalme Salman ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Naibu Mrithi Kiti cha Ufalme, Mohammad bin Salman ametoa amri ya kupiga marufuku wageni kumtembelea baba yake ambaye ana maradhi sugu ya kiakili.