-
Vita vya "Saifel Quds" na maafa yake kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
May 15, 2021 00:00Siku kadhaa zimepita tangu kuanza vita vya Israel na muqawama wa Palestina vinavyojulikana kwa jina la "Saifel Quds" na ingawa kutokana na ukatili wake usio na kifani, utawala wa Kizayuni unasababisha hasara kuwba za roho na mali za Wapalestina kwa kushambulia makazi ya watu, lakini vita hivyo ni kengele ya hatari kwa Israel kwa ushahidi mbalimbali.
-
Netanyahu azishukuru Marekani, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kwa kuunga mkono jinai za Israel
May 14, 2021 23:59Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amewashukuru na kuwapongeza marais Joe Biden wa Marekani na Emmanuel Macron wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kwa kuunga mkono utawala huo dhalimu katika jinai unazoendelea kufanya dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Makumi ya Walebanon wavuka mpaka na kuingia Palestina inayokaliwa kwa mabavu
May 14, 2021 23:56Vyombo vya habari vimeripoti kuwa makumi ya Walebanon wamevunja uzio wa mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel na kuingia katika ardhi hizo kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Makundi ya kutetea haki za binadamu yapinga uamuzi wa Ufarasa wa kupiga marufuku maandamano dhidi ya Israel
May 14, 2021 08:07Wanaharakati na makundi ya kutetea haki za binadamu yamepinga uamuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa wa kupiga marufuku maandamano ya kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya watu wa Palestina ambayo yamepangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
-
Arsenal yamtetea Elneny kwa kuwaunga mkono Wapalestina, yasema wachezaji wana haki ya kueleza maoni yao
May 14, 2021 05:30Klabu ya soka ya Arsenal nchini Uingereza imemtetea mchezaji wake Muislamu raia wa Misri, Mohamed Elneny aliyetuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akiwaunga mkono na kueleza mshikamano wake na watu wa Palestina wanaoendelea kushambuliwa na kuuawa na jeshi la utawala haramu wa Israel.
-
Hania awataka Waislamu, watu huru duniani kutetea Msikiti wa al Aqsa
May 14, 2021 04:28Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameutaka Umma wa Kiislamu na Kiarabu kufanya maandamano na mikutano ya kutetea na kuunga mkono Msikiti wa al Aqsa na watu wa Palestina.
-
Wazayuni wakiri kipigo, wameshapata hasara ya dola milioni 160 kwa mashambulio ya muqawama
May 13, 2021 07:23Chama cha Wazalishaji Bidhaa cha utawala wa Kizayuni kimetangaza kuwa, tangu yalipoanza mashambulizi ya makombora wanamapambano wa Palestina siku chache zilizopita hadi hivi sasa, sekta ya uzalishaji bidhaa ya Israel imeshapata hasara ya dola miliioni 160.
-
Maelfu ya Wapalestina washiriki katika Sala ya Idul Fitr kwenye Msikiti wa al Aqsa
May 13, 2021 07:07Makumi ya maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr leo Alkhamisi asubuhi katika Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu licha ya sheria kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni ambao siku chache zilizopita wanajeshi wa utawala huo katili waliwashambulia kwa mabomu Waislamu waliokuwa wanasali ndani ya Msikiti huo.
-
Mahmoud Abbas: Taifa la Palestina litaendelea kuilinda Quds kwa kupambana na wavamizi
May 13, 2021 01:59Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa Quds ni mstari mwekundu na mji mkuu wa milele wa Palestina na amesisitiza uilazima wa kuendelea kutetea haki za taiifa la Palestina kwa kukabiliana na wavamizi wa Kizayuni.
-
Israel yakataa pendekezo la UN la kusitisha mashambulizi dhidi ya Wapalestina
May 12, 2021 06:01Duru za Palestina zimeripoti kuwa, utawala haramu wa Israel umekataa pendekezo la mjumbe wa Umoja wa Mataifa la kusitisha mashambulizi mara moja dhidi ya watu wa Palestina.