-
Makumi ya watu wafariki dunia katika msongano Kerman, maziko ya Luteni Jenerali Soleimani yanaendelea
Jan 07, 2020 11:39Watu wasiopungua 52 wamefariki dunia mjini Kerman, Iran na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika mkanyagano kwenye shughuli ya kuuaga na kuusindikiza mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani pamoja na mashahidi wengine wa muqawama.
-
Sisitizo la Erdogan la kutoyumkinika mauaji ya kigaidi ya shakhsia kama Kamanda Soleimani kuachwa bila ya jibu
Jan 07, 2020 04:27Wimbi kubwa la kauli, matamko na misimamo ya viongozi na shakhasia mbali mbali wa kimataifa pamoja na maandamano ya upinzani ya wananchi, vinaendelea kushuhudiwa katika nchi za eneo na zingine duniani kuhusiana na mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali shahidi Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Bintiye Shahidi Soleimani: Jina la Haj Qassem Soleimani linawatia kiwewe Wazayuni, Wakufurishaji na Mabeberu
Jan 06, 2020 13:43Bintiye Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: "Baba yangu aliwakosesha usingizi madhalimu wote, madikteta na wakufurishaji. Jina la Haj Qassem Soleimani sasa pia linawatia kiwewe Wazayuni, wakufurishaji na mabeberu."
-
Answarullah ya Yemen: Damu ya Jenerali Qasem Soleimani imeainisha njia ya kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo
Jan 06, 2020 13:37Salim Al-Mughlis, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah ya nchini Yemen amesema kuwa shahidi Qassem Soleimani ameainisha njia ya kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo hili.
-
Mamilioni ya Wairani wauaga mwili wa Jenerali Qassem Soleimani na mashahidi wenzake
Jan 06, 2020 13:22Marasimu ya kuuaga mwili wa shahidi Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, yamefanyika kwa kuhudhuriwa na mamilioni ya watu mjini Tehran.
-
Korea Kaskazini yatoa radiamali yake kufuatia kuuawa kigaidi na Marekani Jenerali Soleimani
Jan 06, 2020 13:15Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vimetoa radiamali kufuatia kuuawa shahidi na askari magaidi wa Marekani Luteni Jenerali Qassem Soleimani na kuitaja Washington kuwa muhusika mkuu wa ongezeko la mizozo katika eneo la Asia Magharibi.
-
Kiongozi wa kidini Pakistan ataka ulipizaji kisasi dhidi ya Marekani kwa damu ya Jenerali Soleimani
Jan 06, 2020 13:08Mmoja wa viongozi wakubwa wa kidini nchini Pakistan amesisitizia ulazima wa kulipizwa kisasi kwa damu iliyomwagwa na Marekani ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani.
-
Sababu na taathira za mauaji ya kigaidi ya kamanda Qassem Soleimani kwa mtazamo wa Sayyid Hassan Nasrullah
Jan 06, 2020 11:12Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah amebainisha sababu, matokeo na taathira za jinai iliyofanywa na Marekani, ya kumuua kigaidi kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Naibu Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq Abu Mahdi Al-Muhandis pamoja na wanamuqawama wengine kadhaa; na akasisitiza kwamba, jinai hiyo ya Washington itapelekea kuanza historia mpya Asia Magharibi.
-
Kiongozi Muadhamu asalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Soleimani na mashahidi wenzake + Video
Jan 06, 2020 08:16Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi amesalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na mashahidi wenzake waliouliwa kigaidi na Marekani nchini Iraq, usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020.
-
Rouhani: Inabidi tusimame imara katika kukabiliana na uingiliaji wa Marekani
Jan 06, 2020 08:15Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, usiku wa kuamkia leo amefanya mazungumzo ya simu na Rais Barham Salih wa Iraq na kusisitiza kuwa, ni jambo zito mno kwa mataifa makubwa ya Iran na Iraq kuweza kuvumilia mauaji ya kigaidi waliyofanyiwa Alhaj Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis na wanamapambano wenzao waliokuwa wamefuatana nao.