-
Hatua ya kwanza nchini Iraq, mwanzo wa historia mpya magharibi mwa Asia
Jan 06, 2020 08:15Bunge la Iraq jana lilipasisha muswada wa kuwafukuza askari wa Marekani nchini humo. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wito uliotolewa na wananchi, wanasiasa na makundi mbalimbali ya Iraq baada ya jeshi la Marekani kumuua kigaidi Jemedari Qassem Solaimani na naibu kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hashdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes.
-
Iran: Marekani ikitushambulia tutaingamiza Israel na kuifuta katika uso wa dunia
Jan 06, 2020 08:14Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika maombolezo ya kukumbuka kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani; Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kwamba, iwapo Marekani itatekeleza vitisho vinavyotolewa na Trump vya kuishambulia Iran, basi wawe na yakini kwamba miji ya Haifa na Tel Aviv na maeneo mengine muhimu ya Israel yataangamizwa kikamilifu na kusawazisha na ardhi.
-
Waziri Mkuu wa Iraq: Soleimani alikuwa mgeni wangu rasmi aliyekuja na ujumbe wa Saudi Arabia
Jan 06, 2020 08:13Kaimu Waziri Mkuu wa Iraq, Adel Abdul Mahdi amesema kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani alielekea nchini Iraq akiwa mgeni rasmi wa serikali na alikwenda na ujumbe wa Saudi Arabia kuhusu mazungumzo.
-
Ismail Hania ametoka Ghaza kuja Tehran kushiriki maziko ya Kamanda Soleimani; asema Soleimani ni shahidi wa Quds + Video
Jan 06, 2020 08:13Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametilia mkazo wajibu wa kuendelea na muqawama hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran; Ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani
Jan 06, 2020 02:40Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Kamanda Qassem Soleimani; na watu wote wanapaswa kutekeleza majukumu yao mbele ya jinai hiyo.
-
Muqtada al-Sadr: Ubalozi na kambi zote za kijeshi za Marekani nchini Iraq zipigwe kufuli mara moja
Jan 05, 2020 16:26Muqtada al-Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Al-Sadr ya nchini Iraq ametoa ujumbe leo kwenda kwa spika wa bunge akitaka kupigwa kufuli ubalozi wa Marekani na kambi zake za kijeshi nchini humo.
-
Nasrullah: Siku ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani, mwanzo wa historia mpya Mashariki ya Kati + Video
Jan 05, 2020 15:56Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Mwili wa shahidi Qassem Soleimani na ya mashahidi wenzake yasindikizwa na kuagwa Ahvaz na Mashhad + Video
Jan 05, 2020 15:40Mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na ya mashahidi wenzake waliouliwa shahidi pamoja naye katika jinai ya kinyama iliyofanywa na majeshi ya kigaidi ya Marekani imesindikizwa na kuagwa leo katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mwa Iran na huko Ahvaz kusini mwa nchi.
-
Malaysia: Marekani imetangaza vita kwa kumuua shahidi Soleimani
Jan 05, 2020 07:38Baraza la Shura la Jumuiya ya Waislamu Malaysia limelaani vikali hatua ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.
-
Hatua ya kijinai ya Trump ni katika juhudi zake za kukwepa kusailiwa
Jan 05, 2020 04:30Gazeti la New York Times la nchini Marekani limechapisha makala inayosema kwamba, amri ya Rais Donald Trump ya kumuua Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC, ilitolewa kwa lengo la kukwepa kusailiwa.