-
Pakistan yatoa radiamali kali kufuatia hujuma ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Qassem Soleimani
Jan 05, 2020 04:29Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesema kuwa, kitendo cha kigaidi kilichofanywa na Marekani cha kumuua shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, kitasababisha ukosefu wa amani katika eneo.
-
Maelfu ya Waislamu nchini India waandamana kulaani kuuliwa shahidi Qassem Soleimani
Jan 05, 2020 04:29Maelfu ya Waislamu nchini India wamelaani vikali kitendo cha Marekani cha kumuua kigaidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC.
-
Taathira za kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis
Jan 05, 2020 04:28Usiku wa manane wa kuamkia juzi Ijumaa Januari 3 viongozi wa Marekani walitekeleza kitendo cha kijinai na kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa kundi la wapiganaji wa kujitolea wa Iraq (Hashdu al Shaabi).
-
Umati mkubwa wausindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani mjini Baghdad
Jan 04, 2020 12:42Umati mkubwa wa watu umejitokeza leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad kushiriki shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH), aliyeuawa shahidi usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.
-
Wapalestina: Sehemu kubwa ya juhudi za Shahidi Soleimani zilihusu ukombozi wa Palestina
Jan 04, 2020 07:45Brigedi za shahidi Izzuddin-al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alielekeza sehemu kubwa ya juhudi zake kwa ajili ya kuutokomeza na kuuangamiza utawala wa Kizayuni na kuhitimisha kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Balozi wa Iran UN: Jibu la mauaji ya kigaidi ya Jenerali Soleimani litakuwa la hatua ya kijeshi
Jan 04, 2020 07:16Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, jibu la mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani yaliyofanywa na Marekani bila shaka litakuwa la hatua ya kijeshi.
-
Wairaqi walaani vikali kuuawa Qassem Soleimani na Abu Mahdi
Jan 04, 2020 02:50Shakhasia mbali mbali wa kisiasa na kidini nchini Iraq wamelaani vikali hujuma ya kigaidi ya Mareknai ambayo imepelekea Meja Jenerali Qassem Suleimani na Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq (Al Hashd al Shaabi) Abu Mahdi la Muhandis kuuawa shahidi.
-
Bei za mafuta na dhahabu zapanda duniani kufuatia mauaji ya Jenerali Soleimani
Jan 03, 2020 12:15Bei za mafuta na dhahabu katika soko la kimataifa kote duniani zimepanda kufuatia kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran, Meja Jenerali Qassem Soleimani.
-
Kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassim Solaimani; mfano wa wazi wa jinai za kivita za Marekani
Jan 03, 2020 11:53Meja Jenerali Qassim Solaimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al Muhandes, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha al-Hashdul al-Shaabi, wameuawa shahidi usiku wa kuamkia Ijumaa ya leo katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mji mkuu wa Iraq.
-
Joe Biden amkosoa vikali Trump kwa kutoa amri ya kuuliwa Jenerali Soleimani
Jan 03, 2020 08:35Joe Biden ambaye ni miongoni ma wanasiasa wa chama cha Democratic wanaochuana kupata tiketi ya kuwakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao wa rais utakaofanyika mwaka huu nchini Marekani amemkosoa vikali Rais Donald Trump kwa kutoa amri ya kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Meja Jenerali Qassem Soleimani.