-
Viongozi wa Misri na Qatar wakaribisha mazungumzo ya Iran na Marekani nchini Oman
Apr 15, 2025 03:16Rais wa Misri na Amir wa Qatar wametoa taarifa baada ya mazungumzo yao huko Doha, mji mkuu wa Qatar na kukaribisha mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani huko Oman.
-
Hatimaye makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza yameanza kutekelezwa
Jan 19, 2025 13:07Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kuwa makubaliano ya kusitisha vita katika Ukanda wa Ghaza yameanza kutekelezwa.
-
Mabadilishano ya kibiashara kati ya Iran na Qatar yaongezeka kwa 53%
Jan 09, 2025 11:29Mabadilishano ya kibiashara kati ya Qatar na Jamahuri ya Kiislamu ya Iran yameongezeka kwa kasi katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
-
Iran na Qatar zasisitiza kuzuiwa mashambulio ya Israel dhidi ya miundomsingi ya Syria
Dec 12, 2024 11:08Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar wamesisitiza juu ya ulazima wa kufanyika juhudi na kuchukuliwa hatua za dhati ili kusimamisha mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya miundomsingi ya Syria na kukalia kwa mabavu maeneo zaidi ya nchi hiyo na utawala huo ghasibu.
-
Rais Pezeshkian: Kuenea ugaidi Syria si kwa manufaa ya nchi yoyote ya eneo hili
Dec 03, 2024 02:51Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na Amir wa Qatar na kusisitiza kuwa, kuenea machafuko na vitendo vya kigaidi nchini Syria si kwa manufaa ya nchi yoyote ya eneo hili, hivyo ni wajibu wa nchi zote kushirikiana kupambana na vitendo hivyo vya kigaidi.
-
Iran na Qatar zasisitiza ulazima wa kuhitimishwa mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza
Nov 21, 2024 07:57Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar katika mazungumzo yao mjini Tehran wamesisitiza juu ya ulazima wa kukomeshwa mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
-
Qatar yaonya kuhusu kupigwa marufuku UNRWA
Nov 16, 2024 13:25Serikali ya Qatar imeonya kuhusiana na hatua ya kupigwa marukufu shughuli za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) na kusisitiza udharura wa kuheshimiwa haki za Wapalestina.
-
Qatar yakadhibisha madai ya kufunga ofisi ya HAMAS mjini Doha
Nov 10, 2024 07:20Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar amepuuzilia mbali ripoti za baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kufungwa kwa ofisi ya Harakati ya Muqawamawa wa Kiislamu ya Palestina HAMAS mjini Doha.
-
Iran yaendelea na jitihada za kusimamishwa vita Ghaza na Lebanon
Oct 31, 2024 07:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Misri, Indonesia na Qatar na kujadiliana nao masuala ya kikanda na uhusiano wa pande mbili ikiwa ni muondelezo wa jitihada za Iran za kuhakikisha vita vinakomeshwa huko Ghaza na Lebanon.
-
Qatar: Hatutaruhusu ardhi, anga yetu zitumike kushambulia majirani
Oct 16, 2024 07:08Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema nchi yake kamwe haitaruhusu Kambi ya Anga ya Al Udeid ambayo ina wanajeshi wa Marekani, Uingereza na Qatar kutumika kufanya mashambulizi dhidi ya nchi za eneo hili la Asia Magharibi.