-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Russia na Uturuki wakutana New York kujadili mgogoro wa Syria
Sep 24, 2023 03:15Sambamba na juhudi zinazoendelea za kidiplomasia za kuushughulikia mgogoro wa Syria, mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Russia na Uturuki wamefanya mkutano wa pande tatu katika muktadha wa Mazungumzo ya Astana kwa ajili ya kujadili njia za kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Hatua mpya ya Russia ya kutumia sarafu za kitaifa na kupunguza utegemezi kwa dola ya Marekani
Sep 23, 2023 02:18Serikali ya Russia imeidhinisha orodha ya nchi 31, zikiwemo Iran, Brazil, Venezuela na Cuba, ambazo benki zao zinaweza kushiriki na kufanya biashara katika soko la fedha za kigeni nchini Russia.
-
Waziri wa Ulinzi wa Russia: Uhusiano na Iran 'unafikia kiwango kipya' licha ya vikwazo
Sep 21, 2023 02:54Waziri wa Ulinzi wa Russia, Jenerali Sergei Shoigu anasema uhusiano wa nchi hiyo na Iran "unafikia kiwango kipya" kinyume na kampeni ya mashinikizo ya Magharibi inayolenga nchi zote mbili.
-
Raisi: Ukraine haijawasilisha ushahidi wa madai ya kutumwa silaha za Iran kwa Russia wakati wa vita
Sep 14, 2023 11:13Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Waukraine wameshindwa kuwasilisha nyaraka zozote zinazoonyesha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iliipatia silaha Russia wakati wa vita.
-
Russia yatungua droni 8 za Ukraine karibu na Crimea
Sep 10, 2023 10:35Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema mifumo ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo imefanikiwa kutungua ndege nane zisizo na rubani (droni) za Ukraine zilizokuwa zinaruka katika anga ya Bahari Nyeusi karibu na eneo la Crimea.
-
Kupungua uzalishaji wa viwanda nchini Ujerumani; sababu na matokeo yake
Sep 09, 2023 10:52Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani imeripoti kwamba uzalishaji wa viwanda nchini Julai iliyopita ulishuka kwa kasi kuliko ilivyotarajiwa, na hivyo kuweka wazi matatizo yanayoukabili uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya.
-
Moscow: Marekani inatafakari kuwaua viongozi wa mapinduzi Niger
Sep 08, 2023 07:19Shirika la Kijasusi la Russia nje ya nchi (SVR) limeonya kuwa, serikali ya Marekani inatafakari suala la kuwaua kigaidi viongozi walioongoza mapinduzi ya kijeshi nchini Niger.
-
Russia: Askari 66,000 wa Ukraine wameuawa katika kujibu mashambulio yetu
Sep 06, 2023 03:13Waziri wa Ulinzi wa Russia ameashiria mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa na Ukraine dhidi ya maeneo ya raia nchini humo na kutoa takwimu za vifo na hasara za uharibifu ilizopata Kiev katika operesheni ilizotekeleza kujibu mashambulio ya Moscow.
-
Hatua mpya ya Marekani ya kukoleza moto wa vita: Kuipelekea Ukraine risasi zenye madini ya urani
Sep 03, 2023 08:49Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani imeamua kwa mara ya kwanza kuipatia Ukraine risasi zenye madini ya urani hafifu. Risasi hizo ni sehemu ya shehena mpya ya silaha ambayo itatangazwa mnamo siku zijazo.
-
Veto ya Russia yazima vikwazo vya UN dhidi ya Mali
Sep 01, 2023 03:04Russia imetumia kura yake ya turufu kuzuia pendekezo la Ufaransa la kurefusha muda wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mali.