-
Kremlin: Kuanzisha chombo bora badala ya Baraza la Usalama la UN kunahitaji mwafaka wa kimataifa
Nov 01, 2023 04:39Msemaji wa Ofisi ya Rais wa Russia amekiri kwamba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kutekeleza majukumu yake. Dmitry Peskov ameyasema hayo akijadili fikra zilizopendekezwa kuhusu udharura wa kuanzishwa taasisi yenye ufanisi badala ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Kushtadi mvutano baina ya Russia na utawala wa Kizayuni wa Israel
Oct 30, 2023 23:05Mvutano baina ya Russia na utawala ghasibu wa Israel umeshadidi baada ya ziara ya wawakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) mjini Moscow.
-
Umati wa watu wenye hasira wavamia uwanja wa ndege Russia kuzuia ndege za Israel zisitue
Oct 30, 2023 10:41Mamia ya watu wenye hasira wamevamia uwanja mkuu wa ndege katika eneo la Dagestan nchini Russia, wakipinga kutua ndege zinazotoka Israel wakati utawala huo haramu wa Kizayuni ukiwa unaendeleza mauaji ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Ndege za kivita za Russia zashambulia maficho ya magaidi Idlib na Latakia nchini Syria
Oct 30, 2023 08:04Naibu mkuu wa Kituo cha Maridhiano cha Russia nchini Syria ametangaza kuwa jeshi la anga la Russia limefanya shambulio dhidi ya maficho ya chini ya ardhi ya makundi ya kigaidi katika miji ya Idlib na Latakia kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
-
Kupigiwa kura ya veto maazimio yanayohusu vita vya Ghaza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Oct 27, 2023 03:57Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena limeshindwa kupasisha azimio Katika hali ambayo wananchi wa Ukanda wa Ghaza bado wanakabiliwa na mashambulizi ya kinyama na ya kutisha ya utawala wa Kizayuni ambapo utawala huo unazuia kufikishwa misaada ya dharura katika eneo hilo.
-
Russia: Marekani haitakuwa tena mhimili mkuu katika "utaratibu mpya wa dunia"
Oct 24, 2023 11:39Russia imekosoa matamshi ya rais Joe Biden wa Marekani kwamba Washington lazima iwe ndiyo nguvu inayoongoza katika "utaratibu mpya wa dunia", ikisema maono kama hayo ya "Marekani kuwa mhimili mkuu" yamepitwa na wakati.
-
Russia yaomba kuitishwa kikao kingine cha Baraza la Usalama la UN kujadili mauaji ya watu wa Gaza
Oct 23, 2023 04:18Russia imeomba kuitishwa tena kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili vita vya Gaza.
-
Balozi wa Korea Kaskazini nchini Russia: Marekani itashindwa huko Ukraine kama ilivyofeli Afghanistan
Oct 21, 2023 23:50Balozi wa Korea Kaskazini nchini Russia amelaani uungaji mkono na misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine na kusema, mara hii pia Marekani itashindwa na kufeli kama ilivyokuwa huko Afghanistan.
-
Ushirikiano wa Korea Kaskazini na Russia dhidi ya Marekani
Oct 21, 2023 07:58Katika mazungumzo yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, wamejadiliana kuhusu uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wao wa hivi sasa na kusisitiza juu ya makubaliano yao ya kutatua kidiplomasia masuala yenye utata katika Peninsula ya Korea.
-
Ukosoaji wa Russia kwa siasa za uadui za Marekani ulimwenguni
Oct 21, 2023 03:54Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Russia amekosoa vikali siasa za uhasama za Marekani ulimwenguni.