-
Padri Mfaransa atuhumiwa kuwadhalilisha kingono wakimbizi watoto
Nov 05, 2025 03:06Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki la Rabat nchini Morocco jana aliliambia shirika la habari la AFP kuwa "ameshirikiana kikamilifu" na mamlaka za Morocco na nje ya nchi baada ya kasisi wa Ufaransa kutuhumiwa kwa kuwadhalilisha kingono wakimbizi watoto huko Casablanca.
-
Ufaransa yatangaza kuwa tayari kutuma wanajeshi nchini Ukraine
Oct 26, 2025 10:19Pars Today- Mkuu wa Komandi Kuu ya Jeshi la Ufaransa ametangaza kwamba ikiwa Russia na Ukraine zitafikia makubaliano ya kusitisha mapigano, Paris itakuwa tayari kutuma wanajeshi nchini Ukraine kama sehemu ya kutoa dhamana za usalama kutoka kwa nchi za Magharibi.
-
Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Sebastien Lecornu ajiuzulu
Oct 06, 2025 11:32Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekubali kujiuzulu Waziri Mkuu aliyemteua hivi karibuni baada ya kukosolewa kuhusu safu ya baraza lake la mawaziri.
-
Sarkozy ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa uhalifu
Sep 26, 2025 02:29Mahakama ya Paris jana Alhamisi ilimhukumu rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kifungo cha miaka mitano jela baada ya kumpata na hatia ya njama ya uhalifu katika kesi aliyotuhumiwa kwamba kiongozi zamani wa Libya mwendazake Muammar Gaddafi alisaidia kufadhili kampeni za Sarkozy katika uchaguzi wa rais mwaka 2007.
-
Polisi yawatia mbaroni watu 295 huku vuguvugu la 'Zuia kila kitu' likiitikisa Ufaransa
Sep 11, 2025 07:19Waandamanaji nchini Ufaransa jana Jumatano walifunga barabara, kuwasha moto na kukabiliana na polisi katika siku ya kwanza ya vuguvugu la harakati ya nchi nzima ya 'Zuia Kila Kitu'.
-
Mediapart: 2024 Israel iliweka 'rekodi ya mwaka' ya ununuzi wa silaha kutoka Ufaransa
Sep 06, 2025 06:18Uuzaji wa silaha wa Ufaransa kwa utawala wa kizayuni wa Israel katika mwaka uliopita wa 2024 ulifikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka minane iliyopita sambamba na kuwepo ongezeko kubwa la mauzo ya silaha za Ufaransa duniani kote. Hayo ni kwa mujibu wa gazeti la ripoti za uchunguzi nchini humo la Mediapart.
-
Ulaghai wa watawala wa Magharibi; Gaddafi alivyodanganywa na Sarkozy
Sep 05, 2025 02:18Moja ya kesi mashuhuri za ulaghai wa watawala wa nchi za Magharibi ni udanganyifu uliofanywa na Nicolas Sarkozy, rais wa zamani wa Ufaransa dhidi ya Muammar Gaddafi, dikteta wa zamani wa Libya.
-
Tunisia yaijia juu polisi ya Ufaransa kwa kuua raia wake Marseille
Sep 04, 2025 07:36Tunisia imewasilisha malalamiko rasmi kwa Ufaransa, ikilaani mauaji ya raia wa nchi hiyo ya Kiarabu yaliyofanywa na polisi wa Ufaransa katika mji wa kusini wa Marseille.
-
Ufaransa yaharakisha kurejesha turathi za kale za nchi za Kiafrika bila ya kuidhinishwa na Bunge
Aug 06, 2025 03:55Serikali ya Ufaransa inafanya jitihada za kuharakisha kurejesha turathi za kale za nchi za Kiafrika katika nchi ilizozikoloni.
-
Ulaya kuitambua rasmi Palestina ni hatua iliyochukuliwa kwa kuchelewa au ni ubadilishaji wa mkakati tu?
Aug 01, 2025 02:45Siku chache baada ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kutangaza kuwa atalitambua rasmi taifa la Palestina katika Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, serikali ya Uingereza nayo pia imesisitiza kuwa hivi karibuni itaitambua nchi ya Palestina.