-
Watu kadhaa wahofiwa kufa katika mlipuko wa bomu Kampala
Oct 24, 2021 03:17Watu asiopungua watatu wanahofiwa kuaga dunia na karibu saba wamejeruhiwa vibaya katika mlipuko wa bomu uliotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo ya Komamboga Jijini Kampala kwenye eneo la kuuzia nguruwe, Tarafa ya Kawempe.
-
Askari wa Uganda kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi kwa kuua raia Somalia
Oct 23, 2021 04:19Mpango wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani nchini Somalia AMISOM umeshauri mahakama ya kijeshi ya Uganda iwafungulie mashtaka askari wa nchi hiyo wanaohudumu katika mpango huo, ambao wamehusishwa na mauaji ya raia nchini Somalia.
-
Uganda kutuma askari polisi 160 wa kulinda amani Somalia
Oct 15, 2021 00:50Uganda inajiandaa kutuma maafisa wa polisi wapatao 160 nchini Somalia, kwenda kushiriki operesheni za kudumisha amani katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Wakimbizi kutoka Afghanistan waanza kuwasili Uganda
Aug 25, 2021 08:27Kundi la kwanza la makumi ya wakimbizi kutoka Afghanistan limewasili nchini Uganda.
-
Uganda yasimamisha shughuli za asasi 54 zisizo za kiserikali
Aug 20, 2021 21:57Serikali ya Uganda imesimamisha shughuli za makumi ya asasi za kirai yakiwemo mashirika ya kutetea haki za binadamu.
-
Chama tawala Uganda chakanusha madai ya kutaka kuingilia uchaguzi wa Kenya
Aug 08, 2021 03:28Chama tawala nchini Uganda cha National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni kimekishutumu vikali chama kikuu cha upinzani nchini Kenya ODM kinachoongozwa na Raila Odinga, kwa kudai kuwa kinalenga kushirikiana na Naibu Rais William Ruto kuibua machafuko ya uchaguzi nchini humo.
-
Watu waghadhibika mno Uganda baada ya wabunge kupatiwa yuro milioni 25 kununulia magari mapya
Jul 25, 2021 03:00Wananchi wa Uganda wameghadhibishwa mno na hatua ya serikali ya kuwapatia wabunge kitita cha yuro milioni 25 kununulia magari mapya ya kifakhari katika nchi hiyo masikini ambayo hivi sasa inahiliki kutokana na janga la dunia nzima la ugonjwa wa Covid-19.
-
Wataalamu wathibitisha raia zaidi ya 800 wa Uganda 'wamedungwa' maji wakiambiwa ni chanjo ya Covid-19
Jul 21, 2021 03:23Mamlaka za serikali ya Uganda zimesema, watu zaidi 800 na idadi kadhaa ya wateja wa makampuni tofauti katika eneo la jiji la Kampala wamedungwa chanjo bandia ya Covid-19.
-
Rais wa Uganda ataka kuimarisha uhusiano wa nchi yake na serikali mpya ya Iran
Jul 04, 2021 09:04Rais wa Uganda amemtumia ujumbe Rais mteule wa Iran, Sayyid Ebrahim Raeisi akimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; huku akieleza kuwa Kampala ipo tayari kuimarisha uhusiano wake na serikali ijayo ya Tehran.
-
Uganda yaidhinisha matumizi ya dawa ya asili 'kutibu Corona'
Jun 29, 2021 21:57Serikali ya Uganda imeidhinisha matumizi ya dawa ya mitishamba ya 'Covidex' kwa ajili ya kutibu magonjwa yanayosababishwa na virusi ukiwemo ugonjwa wa Covid-19.