-
Simulizi ya daktari Mmarekani aliyerejea kutoka Gaza; mauaji makubwa ya kimbari yanajiri katika eneo hilo
Aug 10, 2025 08:53Mark Browner, daktari wa Marekani aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza, amesema katika taarifa yake kwamba mauaji makubwa ya kimbari yanatokea katika eneo hilo na kwamba watu wengi wameaga dunia kwa njaa hivi karibuni katika eneo hilo.
-
Afisa wa UN: Israel inawasababishia njaa kwa makusudi watu wa Gaza
Jul 23, 2025 03:50Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu anasema utawala wa Israel unawaua kwa makusudi watu wa Gaza na kupuuza maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ya kusitisha jinai zake.
-
WHO yasikitishwa na mashambulizi ya Israel dhidi ya wahudumu wake Gaza
Jul 22, 2025 04:24Jeshi la Israel lilishambulia mara tatu makazi ya wafanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika Ukanda Gaza, pamoja na ghala lake kuu jana Jumatatu , amesema mkuu wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa.
-
Umoja wa Mataifa waonya juu ya mgogoro wa njaa Gaza; misaada inaendelea kuzuiwa
Jul 07, 2025 12:01Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeonya kwamba, mfumo wa chakula wa Gaza uko kwenye ukingo wa kuporomoka kabisa, huku hatua ya kuzuiwa msaada wa kibinadamu kuingia katika eneo hilo kukitishia maisha zaidi.
-
Hamas yakaribisha mwito wa BRICS wa kuondoka vikosi vya Israel huko Palestina
Jul 07, 2025 10:50Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imekaribisha kwa mikono miwili wito wa kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi BRICS kwa utawala haramu wa Israel, wa kukomesha vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, na kuondokaa kikamilifu katika eneo hilo la pwani lililozingirwa, na ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Malaki waandamana Hague, Brussels kuonyesha mshikamano na Gaza
Jun 16, 2025 10:22Makumi ya maelfu ya watu waliovalia mavazi mekundu wameandamana katika mitaa ya mji wa Hague nchini Uholanzi na mjini Brussels huko Ubelgiji kuonyesha mshikamano na Wapalestina wa Gaza sanjari na kushinikiza hatua zaidi kutoka kwa serikali zao dhidi ya mauaji ya kimbari katika eneo hilo la Palestina lililozingirwa.
-
Msalaba Mwekundu: Mfumo wa afya wa Gaza 'ni dhaifu mno'
Jun 09, 2025 11:28Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imeonya kuwa, mfumo wa huduma za afya katika Ukanda wa Gaza ni "dhaifu sana" wakati huu ambapo vita vya Israel vinaendelea katika eneo hilo lililozingirwa.
-
"Kuuawa viongozi wa Muqawama kunaimarisha irada ya Wapalestina"
Jun 09, 2025 02:49Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imelaani vikali mauaji ya Israel dhidi ya afisa mashuhuri wa Muqawama na watu wengine 30 katika mji wa Gaza na kusisitiza kuwa, mauaji hayo yanayolenga viongozi wa mrengo wa mapambano kamwe hayatadhoofisha uthabiti na azma ya wananchi wa Palestina.
-
Hamas: Jinai za Israel Gaza zinashinda uhalifu wa Wanazi
Jun 02, 2025 06:44Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amelaani shambulizi la karibuni la Israel dhidi ya wananchi wa Kipalestina wenye njaa waliouawa shahidi wakiendea chakula cha msaada kusini mwa Gaza, akibainisha kwamba mauaji haya yanatuma ujumbe wa wazi kwa ulimwengu wa Kiislamu kwamba wakati umefika wa kusimama dhidi ya wauaji.
-
Israel yaua Wapalestina 30 katika vituo vya misaada vya US, Gaza
Jun 01, 2025 07:15Vikosi vya utawala haramu wa Israel vimewamiminia risasi Wapalestina waliokuwa wamekusanyika katika vituo vya kusambaza misaada vinavyoendeshwa na kundi linaloungwa mkono na Marekani kusini na katikati mwa Gaza, na kuua shahidi takriban 30 miongoni mwao huko Rafah, huku Mpalestina mwingine akiuawa shahidi karibu na korido ya Netzarim.