-
Utafiti: 86% ya Wazayuni hawataki tena kuishi karibu na Gaza baada ya vipigo
Oct 07, 2024 02:19Utafiti mpya wa maoni umefichua kuwa, asilimia 86 ya Waisraeli wanasema hawataishi tena katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko karibu na Ukanda wa Gaza baada ya kumalizika mgogoro huo mbaya zaidi wa kibinadamu uliosababishwa na chokochoko za Tel Aviv.
-
Seneta wa Nigeria: Jinai za Israel Gaza, Lebanon zinaonyesha UN haina maana
Sep 27, 2024 03:05Mwanasiasa wa ngazi ya juu wa Nigeria amesema kuwa, mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon yameonyesha kushindwa kwa dunia kushughulikia suala la Palestina, na pia imeonyesha namna Umoja wa Mataifa ulivyo butu kwa kushindwa kukomesha ukatili na unyama wa Israel.
-
Watoto 625,000 wenye umri wa kwenda shule Gaza wanakabiliwa na sonona
Sep 27, 2024 03:04Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limeripoti kuwa, zaidi ya watoto 625,000 wenye umri wa kwenda shule katika Ukanda wa Gaza wanaandamwa na kiwewe, sonona na msongo mkali wa mawazo huku wakiishi katika magofu na majengo yaliyoharibiwa na mabomu ya Wazayuni.
-
Iran yalaani shambulio la Israel dhidi ya skuli ya UN Gaza
Sep 13, 2024 03:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulizi la anga la Israel dhidi ya shule nyingine iliyogeuzwa makazi na wakimbizi katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 18, wakiwemo wafanyakazi sita wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).
-
Hizbullah: Adui hana chaguo jingine ghairi ya kusitisha vita Gaza
Sep 08, 2024 12:56Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, adui ana njia moja pekee, ambayo ni kusimamisha hujuma na mashambulizi ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Ripoti ya GRFC: Sudan na Gaza ni miongoni mwa maeneo yaliyo katika hatari kubwa ya njaa
Sep 08, 2024 03:08Ripoti iliyotolewa na Shirika la Global Report on Food Crises (GRFC) imeeleza kuwa Nigeria, Sudan, Ethiopia, Zimbabwe, Malawi , Chad na eneo la Ukanda wa Gaza ni maeneo ambayo yapo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na njaa huku Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Lebanon mwaka huu zikipata nafuu ya kiwango fulani ikilinganishwa na mwaka jana wa 2023.
-
Jumuiya ya MSF yailaumu Israel kwa uharibifu unaoendelea mkabala wa mlipuko wa polio huko Gaza
Sep 03, 2024 11:35Kundi la Misaada la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) linalojulikana pia kama Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka limesisitiza kuwa mashambulizi ya Israel na kuharibiwa miundo mbinu ya Ukanda wa Gaza ndio uliosababisha mlipuko wa polio katika eneo hilo.
-
Israel yaendeleza ukatili, yaua Wapalestina 50 ndani ya saa 24 Gaza
Aug 21, 2024 11:51Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza imesema Wapalestina wasiopungua 50 wameuawa shahidi na wengine 124 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya maeneo mbali mbali ya Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.
-
Wazayuni washambulia tena shule na kuua makumi ya watu Gaza
Aug 21, 2024 02:58Mashambulizi ya Israel dhidi ya Shule ya Mustafa Hafez inayohifadhi wakimbizi wa Kipalestina magharibi mwa Ukanda wa Gaza yameua takriban raia 20 na kujeruhi wengine wengi.
-
Muqawama: US ni mshiriki wa mauaji mapya ya halaiki Gaza
Aug 10, 2024 11:13Makundi ya mrengo wa Muqawama katika eneo la Asia Magharibi yamelaani vikali jinai mpya ya kuogofya ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina 100 wameuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa.