UN: Israel inaendelea kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza
-
Farhan Haq
Umoja wa Mataifa umesema Israel inaendelea kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia huko Gaza; mwezi mmoja baada ya kuanza kutekelezwa makualiano ya kusimamisha vita.
Farhan Haq, msemaji wa Umoja wa Mataifa ameinukuu Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) na kusema: Juhudi za kuongeza misaada zinaendelea kukwamishwa, washirika wakuu wa misaada ya kibinadamu wamewekewa marufuku, vivuko na njia za kupitisha misaada zikisalia kuwa chache sana huku ukosefu wa usalama ukishuhudiwa licha ya usitishaji mapigano.
"Amesema, katika baadhi ya maeneo timu za Umoja wa Mataifa zinapasa kuratibu na Israel mapema kila harakati.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa umoja huo unatumia kila fursa kupana oparesheni zake za kibiandamu licha ya kuwepo changamoto mbalimbali. Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu suala la kufungua vivuko zaidi, Farhan Haq amesema: Israel ndiyo inayokwamisha suala hilo.
Israel imewauwa shahidi Wapalestina karibu 70,000 aghalabu yao wakiwa wanawake na watoto katika vita na mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 2023.