-
Trump auza viti vya 'Bodi ya Amani' Gaza dola bilioni 1
Jan 18, 2026 10:24Rais wa Marekani, Donald Trump amezitaka nchi mbali mbali duniani zilipe angalau dola bilioni 1 ili kusalia katika "Bodi ya Amani" ya Gaza, baada ya kumalizika muhula ulioanishwa wa miaka mitatu.
-
Marekani yatangaza wajumbe wa iitwayo 'Bodi ya Amani' ya Ghaza, yumo pia Tony Blair
Jan 18, 2026 02:39Ikulu ya White House imetangaza majina ya wajumbe wa linaloitwa baraza la amani litakaloongozwa na Rais wa Marekani Donald Trump na kusimamia utawala wa eneo la Palestina la Ukanda wa Ghaza. Orodha hiyo inajumuisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mark Rubio, mjumbe maalumu wa Trump Steve Witkoff, mkwe wa Trump Jared Kushner, na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair.
-
Ripoti: Israel inapanga kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Ghaza ifikapo mwezi Machi
Jan 12, 2026 06:02Gazeti la Kizayuni la Times of Israel limeripoti kuwa, jeshi la utawala haramu wa Israel linapanga kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Ukanda wa Ghaza ifikapo mwezi Machi ili kunyakua ardhi zaidi za eneo hilo na kuusukuma Mstari wa Njano kuelekea magharibi zaidi upande wa pwani ya eneo hilo.
-
HAMAS: Tuko tayari kukabidhi uendeshaji wa Ghaza kwa kamati ya shakhsia wa kujitegemea
Jan 10, 2026 02:34Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, harakati hiyo ilishaamua tokea huko nyuma kwamba haitakuwa na ushiriki wa moja kwa moja katika hatua yoyote ya upangaji wa masuala ya kiidara na kiuendeshaji ya siku za usoni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Wizara ya Afya ya Palestina: Waliouawa shahidi Gaza ni zaidi ya 71,300
Jan 09, 2026 06:23Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza katika takwimu zake za hivi karibuni kwamba, Wapalestina zaidi ya 71,000 wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba 2023.
-
Nchi za Waislamu zataka kuruhusiwa misaada ya kibinadamu Gaza
Jan 03, 2026 06:12Mawaziri wa Mambo ya Nje wa mataifa manane ya Waislamu wameitaka jamii ya kimataifa kuishinikiza Israel, kama dola linalokalia kwa mabavu ardhi za Palestina, kuondoa mara moja vizingiti na vikwazo vya kuingia kwa misaada ya msingi na ya dharura katika Ukanda wa Gaza.
-
Al-Jazeera: Israel inajiandaa kuanzisha tena mashambulizi makali Gaza
Jan 03, 2026 02:37Waziri wa Vita wa Israel, Israel Katz ameliagiza jeshi la utawala huo haramu kujiandaa kurejea kwenye mapigano makali dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza, hayo yameripotiwa na kanali ya televisheni ya al-Jazeera ikinukuu gazeti la Kizayuni la The Jerusalem Post.
-
Israel yakemewa, yalaaniwa kimataifa kwa kupiga marufuku asasi 37 zinazotoa misaada Ghaza
Jan 01, 2026 06:03Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani marekebisho ya sheria yaliyopitishwa na Bunge la utawala wa kizayuni wa Israel, Knesset Desemba 29, yanayohusu kusitishwa shughuli za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).
-
Israel yasitisha shughuli za mashirika ya misaada zaidi ya 30 huko Gaza chini ya sheria mpya za usajili
Jan 01, 2026 02:25Israel imesimamisha shughuli za mashirika ya kimataifa 30 ya masuala ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. Waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu wamekosoa na kulaani vikali hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni.
-
Papa Leo azungumzia madhila ya Wapalestina wa Ghaza katika ibada ya Krismasi
Dec 26, 2025 06:30Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amesema katika mahubiri ya Krismasi aliyotoa jana Alkhamisi kwamba anasikitishwa na madhila yanayowafika Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.