-
UN yaiwekea tena Iran vikwazo vilivyokuwa vimeondolewa kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia
Sep 28, 2025 03:51Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeiwekea tena Iran vikwazo vilivyokuwa vimendolewa huko nyuma kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya 2015 katika hatua iliyochochewa na mataifa ya Ulaya bila sababu ya msingi ili kutia dosari miradi ya nyuklia ya Iran, huku baraza hilo likipuuza hatua ya nchi za Magharibi ya kuhujumu makubaliano hayo.
-
Kwa nini Trump anaishupalia jamii ya kimataifa iamini uwongo wake kuhusu Iran?
Sep 27, 2025 07:40Rais wa Marekani kwa mara nyingine tena amekariri katika houba aliyoitoa katika Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa madai yake ya uwongo na yasiyo na msingi dhidi ya Iran.
-
UN, AU na EU zaahidi kushirikiana kwa ajili ya amani na maendeleo barani Afrika
Sep 22, 2025 23:27Viongozi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika AU na Umoja wa Ulaya EU, wametilia mkazo tena dhamira yao ya kuendeleza amani na maendeleo endelevu barani Afrika, kwa kuahidi ushirikiano wa kina zaidi ili kukomesha migogoro, kuimarisha mnepo na kukabiliana na changamoto za kimataifa kuanzia madeni hadi mabadiliko ya tabianchi.
-
Mayahudi wa Othodoksi waanza kuandamana New York dhidi ya Netanyahu kabla hajaelekea UN
Sep 18, 2025 06:43Mamia ya Wayahudi wa madhehebu ya Othodoksi wamefanya maandamano katika jiji la New York kupinga ushiriki wa waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa itakayofanyika wiki ijayo.
-
Wabunge wa UK: Vikosi vya kijeshi vitakavyoongozwa na UN vipelekwe Ghaza kuzuia mauaji ya kimbari
Sep 18, 2025 00:16Wabunge watano wa Uingereza wamemwandikia barua waziri wao wa mambo ya nje Yvette Cooper wakiitaka serikali ya London "ifuatilie kwa dharura uingiliaji kati wa kijeshi utakaoongozwa na Umoja wa Mataifa" ili kukomesha mauaji ya kimbari ya yanayofanywa na Israel huko Ghaza.
-
Baada ya machafuko ya umwagaji damu, Nepal yateua Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke; UN yakaribisha
Sep 13, 2025 07:22Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohudumu nchini Nepal yamekaribisha kuteuliwa Sushila Karki kuwa Waziri Mkuu wa mpito, wakati nchi hiyo ikikumbwa na mshtuko kufuatia ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya maandamano yaliyoongozwa na vijana, ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 50, uharibifu mkubwa wa mali na kujiuzulu kwa mtangulizi wake.
-
Araghchi aikosoa Ulaya kwa kufumbia macho uchokozi wa US, Israel dhidi ya Iran
Sep 12, 2025 03:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi ameyajia juu mataifa matatu ya Ulaya kwa mtazamo wao wa "kutowajibika" mkabala wa uchokozi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel dhidi ya Iran, pamoja na vitisho vyao vya kuhuisha maazimio yaliyobatilishwa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jambo ambalo anaamini litazidisha tu mivutano iliyopo.
-
Kwa nini UN imetoa wito wa kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya makundi ya kutetea haki za binadamu ya Palestina?
Sep 08, 2025 05:28Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, amekosoa vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya makundi ya kutetea haki za binadamu ya Palestina, na kutoa wito wa kuondolewa mara moja.
-
Msimamo wa karibuni wa Malaysia kuhusiana na utawala wa kizayuni na jinai unazofanya Ghaza
Sep 01, 2025 03:54Malaysia imeitaka Jamii ya Kimataifa isimamishe uwanachama wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Umoja wa Mataifa na kuuwekea vikwazo vikali utawala huo ghasibu.
-
Wasia wa ripota Mpalestina aliyeuliwa kigaidi na Israel kwa walimwengu: 'Msiisahau Ghaza'
Aug 11, 2025 07:19Anas al-Sharif, ripota mashuhuri wa chaneli ya Al Jazeera aliyeuliwa shahidi pamoja na wenzake wanne katika shambulio la makusudi lililofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel kwenye hema la waandishi wa habari katika Mji wa Ghaza, amewaomba walimwengu katika wasia wake wasiisahau Ghaza iliyowekewa mzingiro pamoja na watu wa Palestina.