-
UNICEF: Watoto wanafariki Ghaza kwa kasi ambayo 'haijawahi kushuhudiwa'
Aug 02, 2025 09:46Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limeitaka jamii ya kimataifa ichukue hatua za haraka ili kuzuia vifo vingi vya watoto katika Ukanda wa Ghaza, ambako hali inaendelea kuwa mbaya wakati huu wa vita vinavyoendelezwa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya eneo hilo uliloliwekea mzingiro.
-
Maafisa wa Uingereza na Umoja wa Mataifa waitaka London kulitambua rasmi taifa la Palestina
Jul 24, 2025 08:39Zaidi ya maafisa 50 wa zamani wa Uingereza na Umoja wa Mataifa wamemwandikia barua Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer wakimtaka alitambue rasmi taifa la Palestina.
-
UN yasema SDG hatarini kuweza kufikiwa katika anga ya kisiasa iliyopo
Jul 22, 2025 14:36Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa dunia kuongeza kasi na dhamira ya kweli katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanayofikia ukomo wake 2030, akisisitiza kuwa malengo hayo yako hatarini kuweza kufikiwa katika anga ya kisiasa iliyopo hivi sasa duniani.
-
WFP: Theluthi moja ya watu wa Ghaza hawajala kwa siku kadhaa kutokana na mzingiro wa Israel
Jul 22, 2025 06:35Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa, theluthi moja ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza hawajala kwa siku kadhaa kutokana na mzingiro unaoendelea kuwekwa na utawala wa kizayuni wa Israel kwenye eneo hilo la Palestina.
-
Katibu Mkuu wa UN apongeza makubaliano ya amani ya DRC na M23
Jul 21, 2025 03:11Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amekaribisha kwa mikono miwili hatua ya kutiwa saini kwa Azimio la Kanuni kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi la waasi la M23.
-
Iran yakanusha ‘madai hewa’ ya US kuhusu hali ya Yemen na Bahari Nyekundu
Jul 17, 2025 07:19Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ametupilia mbali tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Marekani dhidi ya Iran kuhusu hali ya Yemen na Bahari Nyekundu akisema "hazina msingi wowote" na akalaani ushiriki wa kijeshi wa Washington katika hujuma dhidi ya Yemen.
-
Unajua kwa nini Marekani imemuwekea vikwazo Ripota Maalumu wa UN kuhusu Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa kwa Mabavu?
Jul 10, 2025 22:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alitangaza Jumatano, Julai 9, kwamba atamuwekea vikwazo Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa kwa Mabavu, kwa kile alichokiita "juhudi zisizo halali zinazohusiana na uchunguzi wake kuhusu vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza" na eti kwa kuchukua "hatua dhidi ya maafisa wa Marekani na Israel."
-
Umoja wa Mataifa 'washtushwa' na mauaji ya waandamanaji Kenya
Jul 08, 2025 10:50Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi mkubwa juu ya vifo vya watu zaidi ya 10 nchini Kenya, ambapo polisi na waandamanaji walikabiliana wakati wa maandamano ya kupinga sera za serikali ya nchi hiyo Jumatatu.
-
WFP yadondosha misaada Sudan Kusini kutokea angani kutokana na mapigano
Jul 07, 2025 13:08Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) limeanza kudondosha misaada ya dharura ya chakula kwa njia ya anga kwa maelfu ya familia katika Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, ambako mapigano yaliyopamba moto tangu mwezi Machi mwaka huu yamewafanya watu walazimike kuhama makazi yao na kukaribia kuzitumbukiza baadhi ya jamii kwenye njaa ya kupindukia.
-
Araqchi akosoa kimya cha Baraza la Usalama kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran
Jul 01, 2025 09:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa kimya cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran.