Pars Today
Russia na Venezuela zimechukua hatua nyingine ya kuimarisha uhusiano wao kwa kuanzisha kamisheni ya viongozi wa nchi mbili na vile vile kuanzisha kamisheni tano za pamoja za kiufundi.
Siasa za uingiliaji mambo za Marekani za washirika wake wa Magharibi zingali zinaendelea katika akthari ya nchi za Amerika ya Latini.
Hatua na misimamo ya upande mmoja na kupuuzwa taasisi za kimataifa khususan Umoja wa Mataifa katika kipindi cha utawala wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump vimepelekea kudhoofika umoja huo na hati ya Umoja wa Mataifa.
Kutokana na kuendelea sera za vikwazo za Marekani na madola ya Ulaya, dhidi ya Venezuela, Rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo amesisitiza kuwa, nchi yake itaendelea kusimama kidete mkabala wa sera hizo ambazo amesema kuwa ni “vita vya kiuchumi vya pande kadhaa”.
Viongozi wa Caracas wamelaani "vita vya kiuchumi vya pande kadhaa" za Umoja wa Ulaya na Marekani dhidi ya Venezuela.
Rais wa Venezuela ametangaza kuwa, shambulio la kigaidi limejiri katika bomba la mafuta la shirika la mafuta na gesi la serikali la Petroleus de Venezuela na kulaani shambulio hilo ambalo limesababisha moto mkubwa.
Rais wa Venezuela amekutaja kuondoka huko White House Rais wa zamani wa Marekani kuwa ushindi kwa nchi yake.
Baada ya Donald Trump kubwagwa katika uchaguzi wa rais wa Novemba 3, 2020 huko Marekani, sasa wafuasi, mashabiki na vibaraka wake wa nje, nao wameanza kuonja makali ya kuwa vibaraka wa Marekani.
Katika kuanza mwaka mpya wa 2021 Miladia Rais wa Venezuela akiashiria suala la kuilinda ardhi ya nchi hiyo amesisitiza kuwa ataimarisha uhusiano na Iran, Russia, China, Cuba, Uturuki na India.
Licha ya kufeli kwa sera za vikwazo za Marekani dhidi ya Venezuela, lakini viongozi wa Washington wangali wamekumbatia siasa hizo za mashinikizo na kuendelea kutekeleza siasa hizo zilizoshindwa na kugonga ukuta dhidi ya nchi hiyo ya Amerka ya Latini.