Maduro: Nimeifuta WhatsApp kwa sababu inatumika katika ujasusi na mauaji
(last modified Thu, 03 Jul 2025 03:59:46 GMT )
Jul 03, 2025 03:59 UTC
  • Maduro: Nimeifuta WhatsApp kwa sababu inatumika katika ujasusi na mauaji

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema katika mahojiano ya kipindi cha televisheni kwamba messenger ya WhatsApp imekuwa ikitumika kwa shughuli za kijasusi na mauaji ya Wapalestina, na kwamba kwa sababu hiyo amefuta messenger ya WhatsApp.

Amesema nchi yake sasa inatafuta mbadala salama wa mawasiliano badala ya WhatsApp. Rais Nicolas Maduro ametangaza kufuta messenger ya WhatsApp katika simu yake ya rununu. Maduro ameeleza haya katika kipindi cha runinga kinachorushwa kila wiki nchini humo; na kuongeza kuwa programu hiyo imekuwa ikitumika kuwafanyia ujasusi watumiaji wake. 

Rais Maduro aliongeza: "Nimefuta WhatsApp maishani mwangu.

Rais wa Venezuela  ameashiria mashambulizi dhidi ya Wapalestina katika vita vya Gaza na kusema: Jukwaa hili linatumiwa kubaini makazi ya ili kutekeleza mauaji." 

 WhatsApp imekuwa ikitumika kuwashambulia na kuwauwa Wapalestina.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Maduro kuikosoa WhatsApp. Mwezi Septemba mwaka jana alisema kuwa programu hiyo ilijihusisha na masuala ya ujasusi wakati kulipokuwa na mvutano baada ya kufanyika uchaguzi huko Venezuela. 

Ameongeza kuwa "wao WhatsApp wanafahamu kila kitu kuhusu maisha yako". Maduro amekariri kutotumia tena WhatsApp na kuwashauri watumiaji wa mtandao huo kutumia njia nyingine mbadala.

Rais wa Venezuela pia amesema na hapa ninamnukuu: "Walitumia WhatsApp kuwaua wanasayansi wa nyuklia nchini Iran waliokuwa wakitafiti katika taaluma za fizikia na hisabati.