Baqaei alaani vikali kuwekewa vikwazo wanadiplomasia wa Iran mjini New York
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i131178-baqaei_alaani_vikali_kuwekewa_vikwazo_wanadiplomasia_wa_iran_mjini_new_york
Ismail Baqaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikwali kitendo cha maafisa wa Marekani kuwawekea vikwazo wanadiplomasia wa Iran mjini New York. Wanadiplomasia wa Iran wako nchini Marekani kushiriki
(last modified 2025-09-24T05:59:57+00:00 )
Sep 24, 2025 05:59 UTC
  • Baqaei alaani vikali kuwekewa vikwazo wanadiplomasia wa Iran mjini New York

Ismail Baqaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikwali kitendo cha maafisa wa Marekani kuwawekea vikwazo wanadiplomasia wa Iran mjini New York. Wanadiplomasia wa Iran wako nchini Marekani kushiriki

Baqaei ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: "Lengo halisi la Marekani katika kuweka vikwazo vikubwa dhidi ya wanadiplomasia wa Iran na familia zao huko New York ni kuvuruga shughuli za kidiplomasia za Iran katika Umoja wa Mataifa."

Ameongeza kuwa: "Unyanyasaji wa kimfumo wa wanadiplomasia wa Iran unaofanywa na serikali za Marekani umeizuia Iran kushiriki katika mikutano kadhaa ya kimataifa iliyofanywa nje ya mipaka iliyowekwa na Marekani katika wiki moja tu iliyopita."

Baqaei amesema: "Kuweka vikwazo hivi vya kipuuzi kwenye harakati hata za manunuzi ya bidhaa za kila siku ya wanadiplomasia wa Iran si tu ni ukiukaji mkubwa wa sheria unaofanywa na Marekani chini ya Mkataba wa kuwa mwenyeji wa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, lakini pia kunaonyesha kiwango kipya cha uadui wa utawala wa Marekani dhidi ya Wairani."

Hayo yamekuja huku Rais Masoud Pezeshkian wa Iran akisema kabla ya kuondoka mjini Tehran kuelekea New York Marekani kushiriki katika kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba haiwezekani kuwa na mazungumzo na mtu yeyote ambaye ana nia ya “kulazimisha, kudhulumu, kufanya hila au kuvuruga mambo.”

Akizungumza jana Jumanne jijini Tehran kabla ya safari yake ya kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Pezeshkian amesema mkutano huo ni fursa adhimu kwa viongozi wa dunia kutoa kauli zao na kwa Iran kuwasilisha misimamo yake.