Kuzidi kuharibika uhusiano wa kidiplomasia kati ya India na Canada
https://parstoday.ir/sw/news/world-i102522-kuzidi_kuharibika_uhusiano_wa_kidiplomasia_kati_ya_india_na_canada
India imemfukuza mwanadiplomasia wa Canada ikilipiza kisasi kwa hatua ya Canada kumfukuza mwanadiplomasia wa nchi hiyo. Hii ina maana kwamba, kiwango cha mvutano wa kisiasa na kidiplomasia katika uhusiano wa India na Canada kimeongezeka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 22, 2023 02:31 UTC
  • Kuzidi kuharibika uhusiano wa kidiplomasia kati ya India na Canada

India imemfukuza mwanadiplomasia wa Canada ikilipiza kisasi kwa hatua ya Canada kumfukuza mwanadiplomasia wa nchi hiyo. Hii ina maana kwamba, kiwango cha mvutano wa kisiasa na kidiplomasia katika uhusiano wa India na Canada kimeongezeka.

Kitendo  cha India cha kumfukuza mwanadiplomasia wa Canada kinaonyesha kuwa, New Delhi haikubaliani na shutuma za Ottawa kwamba India ilihusika katika mauaji ya kiongozi wa Wasikh wanaotaka kujitenga nchini humo.  Serikali ya Canada bado inasisitiza kuwa, India ilihusika katika mauaji ya mmoja wa viongozi wa wanaotaka kujitenga katika jimbo la Punjab kwenye ardhi ya nchi hiyo, na kama ishara ya kupinga, imechukua hatua ya kumfukuza mwanadiplomasia wa India. New Delhi imelipiza kisasi dhidi ya hatua ya Ottawa kwa kumfukuza mwanadiplomasia wake.

"Tsu Su Yuzheng", mtaalamu wa masuala ya kimataifa, anasema kuwa: Canada, kama vile  nchi nyingine za Ulaya na   Marekani imekaribisha nchini humo kundi la Sikh Taliban  la wanaotaka kujitenga nchini India ambalo linataka  kuunda nchi inayoitwa Khalstan katika eneo la  kijiografia la India. Canada inatumia mvutano na mgogoro kati ya pande mbili hizo kama fimbo ya kuishinikizo Delhi New. Wakati huo huo,India inafahamu kuwa muundo wa  Canada iko chini ya ufalme wa Uingereza, na  Ottawa inatekeleza sera na siasa za  mfumo mzima wa ufalme huo. 

Justin Trudeau

Siasa hizo zinafuatiliwa kwa karibu sana na serikali ya Canada  na Justin Trudeau, Waziri Mkuu ana nafasi muhimu, katika uwanja huo. Shutuma kali za Waziri Mkuu wa Canada dhidi ya India kuhusu kuuawa kiongozi mashuhuri wa  Sikh katika jimbo la Punjab zinaonyesha umuhimu kwa Canada wa kuwepo kundi  la  wanaotaka kujitenga nchini India nchini humo. Kwa hivyo, radiamali kali ya India  inaonyesha serikali ya New Delhi  haitaruhusu kuchezewa  mvutano na mgogoro wa eneo na umoja wa kitaifa wa India na madola ya magharibi. 

Kwa upande mmoja, Serikali ya India inawatuhumu wanadiplomasia wa Canada  kuingilia kati  masuala ya ndani ya India , na  hatua ya  Wizara ya Mambo ya Nje ya India, ya kumfukuza mwanadiplomasia mkuu wa Canada inaonyesha wasiwasi mkubwa wa India kuhusiana na athari  ya siasa zilizo dhidi yake za Ottawa  kuhusiana na  masula  ya ndani ya nchi hiyo.

Deepa MC Singh, mtaalamu wa masuala ya kisiasa, anasema: "India kwa kuwa na dini nyingi tofauti, rangi na lugha tofauti tofauti inahesabiwa kuwa ni yenye umoja na muungano  mkubwa wa kitaifa. Lakini nchi za magharibi  zinatumia suala la kuunga mkono makundi yanayotaka kujitenga,na  kuyakaribisha makundi ya upinzani kama vile la Sikh kama siasa za kuishinikiza serikali ya India. Kwa kuzingatia historia ya Uingereza katika kuitawala India, ni jambo lilo wazi kwamba serikali ya London iko nyuma ya mvutano kati ya India na Canada. 

Hardeep Singh Nijjar

Kwa vyovyote vile, India, huku ikikataa shutuma za Wacanada kuhusu mauaji ya Hardeep Singh Nijjar, mmoja wa viongozi Sikh wanaodai kutenga  katika  jimbo la Punjab, imemtangaza kuwa gaidi. Kwa hivyo, serikali ya India imeitaka  Canada kuyatokomeza na kuchukua hatua dhidi ya makundi ya kigaidi yanayoeneza  ghasia  India  badala ya kuwatia nguvu moyo 

Inaonekana kwamba serikali ya Canada  imependelea kuwapa himaya makundi yanayotaka kujitenga ya Sikh badala ya kuimarisha ushirikiano wake na New Delhi. Inafaa kuzingatia kuwa Uingereza kama mkoloni mkongwe wa nchi hiyo,wakati wa kuondoka iliacha  mizozo ya mipaka , katika eneo la kijiografia la Bara Hindi kama vile kati ya India na Pakistan, na Pakistan na Afghanistan. Mgogoro wa kujitenga kundi la Sikh na siasa za kuundwa dola la Khalstan ni miongoni mwa sera  jumla za London za kutaka kujitanua au kuidhoofisha serikali ya New Delhi.