Umoja wa Mataifa waonya kuhusu mpango hatari wa Israel dhidi ya watu wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i126694-umoja_wa_mataifa_waonya_kuhusu_mpango_hatari_wa_israel_dhidi_ya_watu_wa_gaza
Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kuonya kwamba mpango mpya wa Israel wa kusambaza misaada huko Gaza umekuwa chombo cha ulaghai na kuwahamisha wakazi wa eneo hilo, na ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu.
(last modified 2025-05-22T12:29:36+00:00 )
May 22, 2025 12:29 UTC
  • Umoja wa Mataifa waonya kuhusu mpango hatari wa Israel dhidi ya watu wa Gaza

Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kuonya kwamba mpango mpya wa Israel wa kusambaza misaada huko Gaza umekuwa chombo cha ulaghai na kuwahamisha wakazi wa eneo hilo, na ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu mpango mpya wa Israel wa kusambaza misaada huko Gaza, ukiutaja kuwa ni chombo cha ulaghai na kuwahamisha wakazi wa Gaza. Suala hili sio tu kwamba, linadhuru hali ya kibinadamu huko Gaza, lakini pia linaweza kuwa na matokeo mapana ya kisiasa na kijamii katika eneo hilo.

Kufuatia ongezeko la mivutano na mgogoro wa kibinadamu huko Gaza, Israel kwa kisingizio cha kusambaza misaada ya kibinadamu imechukua hatua ambazo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zinalenga kuwaondoa kwa nguvu watu wa Gaza. Mpango huu umekabiliwa na upinzani wa kimataifa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu.

Mpango mpya wa Israel unaweza kusababisha kuhama zaidi kwa raia na kuongeza hatari yao.

Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa, Israel ikiwa ni dola inayokalia kwa mabavu, inawajibika kutoa mahitaji ya kimsingi ya maisha kwa raia na lazima ijiepushe na sera za njaa.

Onyo hili la Umoja wa Mataifa linaonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu huko Gaza na athari zake kwa usalama wa kikanda. Kwa kuzingatia kuwa Israel kama utawala unaokalia kwa mabavu una wajibu wa kisheria na kimaadili kwa raia, kushindwa kuzingatia majukumu hayo kunaweza kusababisha kushadidi mgogoro wa kibinadamu na kuongezeka mivutano katika eneo.