Dec 16, 2019 02:33 UTC
  • Jumatatu tarehe 16 Disemba 2019

Leo ni Jumatatu tarehe 19 Rabiuthani 1441 Hijria sawa na Disemba 16 mwaka 2019.

Siku kama hii ya leo miaka 21 iliyopita Mahakama ya Rufaa ya Paris ilimhukumu kifungo na kumtoza faini mwanafalsafa na msomi mashuhuri wa nchi hiyo, Roger Garaudy, kwa kosa eti la kukana jinai dhidi ya binadamu katika kitabu chake cha 'The Founding Myths of Israeli Politics'. Katika kitabu hicho msomi huyo Mfaransa alithibitisha kisayansi na kwa hoja madhubuti kwamba Wazayuni walishirikiana na Manazi katika Vita vya Pili vya Dunia. Vilevile amethibitisha kwa hoja na ushahidi kwamba, kwa shabaha ya kutaka kupata uungaji mkono wa kuunda dola bandia la Israel katika ardhi ya Palestina, Wazayuni walikuza na kutia chumvi kupita kiasi jinai zilizofanywa na Adolph Hitler dhidi ya Mayahudi. Katika kitabu cha 'The Founding Myths of Israeli Politics' Profesa Garaudy anasema, idadi ya Mayahudi milioni 6 inayotajwa na Wazayuni kuwa iliuawa na Wajerumani wa zama za Hitler imetiwa chumvi kupita kiasi kwani jamii ya Wayahudi katika kipindi hicho haikuwa kubwa kiasi hicho. Msomi huyo alikamatwa na kuhukumiwa kifungo nchini Ufaransa kutokana na maoni yake, suala ambalo limethibitisha urongo wa madai ya demokrasia na uhuru wa maoni nchini Ufaransa.

Roger Garaudy

Katika siku kama ya leo miaka 22 iliyopita kanali ya televisheni ya ya Sahar ya Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo cha Shirika la Redio na Televisheni la Iran Ilianza kazi zake kwa kurusha matangazo ya lugha za Kiarabu, Kiazari, Kibosnia, Kituruki, Kifaransa, Kiingereza na Kiurdu. Televisheni za kanali hiyo zinatayarisha na kurusha matangazo mbalimbali yanayolenga familia katika masuala ya kijamii, kisiasa, filamu, sinema za matukio ya kweli, masuala ya kiuchumi na kadhalika. Vilevile televisheni hizo huakisi habari za matukio mbalimbali ya kieneo na kimataifa.

Siku kama hii ya leo miaka 28 iliyopita Kazakhstan ilijitangazia uhuru baada ya kudhihiri dalili za kusambaratika Urusi ya zamani. Wakazaki ambao wanaunda jamii kubwa zaidi nchini humo na ambao ni kutoka makabila ya Waturki na Wamongoli, katika karne ya 17 miladia, waliganyika katika sehemu tatu za tawala kubwa za kisultani. Mwanzoni mwa karne ya 18 taratibu waliwekwa chini ya udhibiti wa Warusi na wakati huo khususan katika karne ya 19 Miladia, Wakazaki hao wakiwa pamoja na watu wa maeneo mengine ya Asia ya kati walijiunga na dini ya Kiislamu.

Bendera yya Kazakhstan

Miaka 69 iliyopita katika siku kama ya leo ilianza harakati ya kupigania uhuru ya watu wa Cyprus kwa shabaha ya kuhitimisha ukoloni wa Waingereza kisiwani humo. Kisiwa cha Cyprus kilichoko katika Bahari ya Miditerranean kiliwekwa chini ya utawala wa Kiothmania katika karne ya 16. Mwaka 1925 Uingereza ilikiunganisha kisiwa hicho na makoloni yake na tangu wakati huo kulitokea mapigano baina wakazi wa kisiwa hicho yaani Waturuki na Wagiriki. Hatimaye Cyprus ilipata uhuru mwaka 1974 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na Wagiriki huku Waturuki wa kisiwa hicho wakidhibiti eneo la kaskazini la nchi hiyo. 

Bendera ya Cyprus