Sep 06, 2020 02:25 UTC
  • Jumapili tarehe 6 Sepemba 2020

Leo ni Jumapili tarehe 17 Mfunguo Nne Muharram mwaka 1442 Hijri sawa na tarehe 6 Septemba 2020.

Miaka 544 iliyopita katika siku kama hii ya leo aliaga dunia Nuruddin Abdul-Rahman Jami, mshairi, arifu na mwanafasihi mkubwa wa Kiirani wa karne ya 9 Hijria huko katika eneo l herat Afghanistan ya leo ambalo wakati huo lilikuwa sehemu ya Iran. Alizaliwa katika mji wa Jam ulioko katika mkoa wa Khorasan kaskazini mashariki mwa Iran. Alianza kujifunza elimu mbalimbali akiwa katika rika la ujana. Alikuwa na mapenzi na itikadi thabiti kwa Watu wa Nyumba ya Bwana Mtume SAW na katu hakuwahi kuwasifu wafalme na masultani..Silsilat al-Dhahab, Nafatul Uns, Shawahidun Nubuwwah na Baharestan ni baadhi ya vitabu vya Nuruddin Abdul Rahaman Jami.

Kaburi la Abdul Rahaman Jami

Siku kama ya leo miaka 254 iliyopita, alizaliwa John Dalton, msomi na mtaalamu wa fizikia wa Kingereza katika familia ya watu wa kijijini. Kutokana na Dalton kupendelea sana elimu na licha ya kukabiliwa na matatizo mengi, alifanikiwa kwenda shuleni na kujifunza mambo mbalimbali. Ni wakati huo ndipo alipoanza kufanya uchunguzi na utafiti katika masuala mbalimbali ya kielimu. Dalton alibuni na kuvumbua mambo mengi katika uwanja wa fizikia, kemia na sayansi asilia baada ya utafiti mkubwa. Msomi huyo hakuchoka na badala yake aliendeleza utafiti mkubwa katika uga atomu. John Dalton alifariki dunia mwaka 1944.

John Dalton

Katika siku kama ya leo miaka 55 iliyopita, jeshi la India lilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Pakistan kufuatia machafuko ya zaidi ya mwezi mmoja katika mipaka ya nchi mbili hizo. Hivyo vilikuwa vita vya pili vikubwa kuwahi kutokea kati ya nchi mbili hizo jirani kuhusiana na eneo la Kashmir. Vita hivyo vilidumu kwa takribani wiki tatu. Pakistan na India zilikubaliana kusimamisha mapigano kufuatia upatanishi wa Urusi ya zamani. Viongozi wa nchi mbili hizo hatimaye waliafikiana kuanza mazungumzo tarehe 10 mwezi Juni mwaka 1966 huko Tashkent mji mkuu wa Uzbekistan nchini ya upatanishi wa Waziri Mkuu wa Urusi ya zamani. Japokuwa azimio la Tashkent lilibainisha njia za kumaliza mgogoro wa eneo la Kashmir na namna ya kuboresha uhusiano kati ya New Delhi na Islamabad na pia kukaribishwa na nchi mbalimbali duniani, lakini lilishindwa kumaliza hitilafu kati ya India na Pakistan kuhusu umiliki wa eneo la Kashmir.

Vita vya pili vya Kashmir

Katika siku kama ya leo miaka 52 iliyopita, nchi ya Kiafrika ya eSwatini (Swaziland) ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza na kila inapowadia siku kama ya leo husherekewa nchini humo kwa anwani ya siku ya taifa. Kuimarika ukoloni wa Ulaya huko kusini mwa Afrika kulisababisha pia eSwatini kukaliwa kwa mabavu na wakoloni wa Ulaya. Hatimaye katika siku kama ya leo nchi hiyo ndogo ya kusini mwa Afrika ilipata uhuru. eSwatini ina ukubwa wa kilomita mraba 17364 na kijiografia iko kusini mwa bara la Afrika ikiwa inapakana na nchi za Msumbiji na Afrika Kusini.

Tarehe 16 Shahrivar miaka 36 iliyopita aliaga dunia Ayatullah Mirza Muhammad Baqir Ashtiyani, mmoja wa maulamaa wakubwa wa Iran. Alizaliwa mwaka 1284 Hijria Shamsiya mjini Tehran. Ayatullah Ashtiyani alielekea katika chuo cha kidini cha Najaf nchini Iraq kwa ajili ya kukamilisha masomo baada ya kuhitimu masomo yake ya awali. Ayatullah Mirza Muhammad Baqir Ashtiyani alirudi Tehran na kuanza kutoa elimu kwa wanafunzi wa masuala ya dini baada ya kupata daraja ya ijtihadi. Msomi huyo mkubwa ameandika vitabu vingi vya thamani kama "Uongozi kwa Mtazamo wa Uislamu" na kile cha "Umiliki katika Uislamu". 

Ayatullah Mirza Muhammad Baqir Ashtiyani