Jun 01, 2023 01:21 UTC
  • Alkhamisi tarehe Mosi Juni mwaka 2023

Leo ni Alkhamisi tarehe 12 Dhilqaada 1444 Hijria sawa na tarehe Mosi Juni mwaka 2023.

Katika siku kama ya leo miaka 363 iliyopita Mary Barrette Dyer, ambaye alikuwa mhubiri wa Quakerism huko Marekani, alinyongwa na mahakama ya Massachusetts kwa sababu za kidini. Wakati huo, sheria ya Massachusetts ilikataza Maquakers kuingia eneo hilo. Wafusi wa kundi hilo wanaojuulikana kama Quakers ni watu waliokuwa katika kundi la kihistoria la Kikristo la Kiprotestanti linalojulikana kama Jumuiya ya Kidini ya Marafiki. Quakerism iliibuka katika karne ya 16 na 17 kama jibu kwa hitilafu na vita vya kidini vilivyotokea huko Ulaya na vilevile uhasama na mizozo baina ya madhehebu ya Kikristo nchini Uingereza. George Fox alikuwa mmoja wa wahubiri mashuhuri wa kundi hilo. Kundi hili lilienea polepole katika ulimwengu wa Kikristo. Quakers waliamini katika kurahisisha shughuli za kidini na kwamba kanisa halipaswi kuwa na mchungaji maalumu na anayelipwa mshahara na kuwa kiunganishi na wasita kati ya Mungu na Mtume wake kwa upande mmoja, na watu wa kawaida kwa upande mwingine. Waliamini kuwa mahubiri na mafundisho ya Kikristo yanapaswa kufanywa kwa hiari na kila mtu mwenye ujuzi. 

Siku kama ya leo tarehe Mosi Juni miaka 71 iliyopita, aliaga dunia John Dewey, msomi na mwandishi mashuhuri wa Marekani. Alihitimu falsafa katika Chuo Kikuu cha Vermont kabla ya kuwa na umri wa miaka ishirini, na baada ya kupata shahada ya uzamivu katika taaluma ya falsafa, alifundisha katika Chuo Kikuu cha Columbia. Dewey alibobea mno katika taaluma ya elimu na malezi. Dewey alifanikiwa kuandika vitabu vingi kuhusiana na elimu na malezi. Miongoni mwa vitabu mashuhuri vya msomi huyo ni pamoja na "How we Think", "The Public and its Problems" na "Freedom and Culture." John Dewey alifariki dunia mwaka 1952 akiwa na umri wa miaka 93.

John Dewey

Miaka 97 iliyopita muwafaka na siku kama ya leo, moja kati ya zilzala kubwa zilizouwa watu wengi duniani, iliikumba Tokyo mji mkuu wa Japan. Zilzala hiyo ilitokea nyakati mbili tofauti kwa kupishana muda mfupi. Mtetemeko huo wa ardhi uliharibu nusu ya mji wa Tokyo na kuuwa watu zaidi ya laki moja na elfu hamsini.