Mar 12, 2016 16:57
Assalaamu Alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika kipindi hiki maalumu nilichokuandalieni kwa mnasaba wa kukumbuka siku aliyokufa shahidi Bibi Fatima Zahra (a.s) binti mtukufu wa Bwana Mtume (s.a.w) na mwanamke bora duniani na akhera, mwanamke ambaye ni kigezo na ruwaza njema.