Jul 07, 2020 08:02
Harakati za muqawama wa Kiislamu za Hamas ya Palestina na Hizbullah ya Lebanon zimepinga vikali mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kutaka kutwaa na kughusubu ardhi ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza kuwa, uporaji huo ni hujuma ya moja kwa moja dhidi ya Wapalestina.