Jun 13, 2020 07:35
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amemkosoa Yousef Al Otaiba Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) mjini Washington, Marekani ambaye anafanya juu chini kutafuta nukta za pamoja baina ya nchi yake na utawala ghasibu wa Israel huku akiomba kuwepo uhusiano wa kawaida baina ya nchi yake na utawala huo.