Pars Today
Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Palestina (Hamas) ameitaka Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) inayoongozwa na Mahmoud Abbas kuchukua uamuzi wa kihistoria na kuungana na makundi na harakati nyingine za kitaifa na Kiislamu za Palestina.
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amelaani mashambulizi ya makombora ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Syria.
Hali ya kiafya ya Muhammad Khidhri, mwakilishi wa harakati ya muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ambaye alitiwa mbaroni miezi kadhaa iliyopita nchini Saudia, imezidi kuwa mbaya.
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema "Muamala wa Karne" unakusudia kusambaratisha kadhia ya Palestina.
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema njama zozote zinazolenga kuufanya wa kawaida uhusiano baina ya mataifa ya Kiarabu na utawala haramu wa Israel ni kosa ambalo halina msahama.
Harakati za Muqawama wa Kiislamu za Palestina HAMAS na Jihadul-Islami zimekosoa vikali mpango wa baadhi ya nchi za Kiarabu wa kutaka kurejea kwenye meza ya mazungumzo na utawala haramu wa Israel.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeutaja mpango wa kuunganisha Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kama njama hatari zaidi ya kuziyahudisha ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Duru mjini Cairo zinadokeza kuwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) inashirikiana na serikali ya Misri katika kukabiliana na magaidi wakufurishaji katika eneo la Sinai.
Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imefanikiwa kutungua ndege isiyo na rubani ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ichukue hatua za dharura za kuzuia hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel kunyakua ardhi zaidi za Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem) na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.