-
Ebrahim Raisi: Sera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutetea madhulumu
Jan 07, 2024 01:02Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, siasa za Iran ni kuwatetea na kuwalinda wanaodhulumiwa na kupaza sauti dhidi ya madhalimu.
-
Ebrahim Raisi: Usalama wa ukanda huu mzima una deni kwa Luteni Jenerali Soleimani
Jan 06, 2024 03:22Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, usalama na amani iliyopo leo katika eneo hili inatokana na jihadi kubwa ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.
-
Iran yafanya mazishi ya pamoja ya wahanga wa ugaidi Kerman; yaahidi kuwasaka magaidi popote walipo
Jan 05, 2024 08:44Wananchi wa Iran leo Ijumaa wamefanya shughuli ya mazishi ya pamoja kwa wahanga wa miripuko miwili ya kigaidi iliyotokea Jumatano katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa nchi huku kamanda wa ngazi ya juu wa Iran akiahidi kuwasaka magaidi popote walipo.
-
Spika: Shahidi Soleimani ni nembo ya umma wa Kiislamu
Jan 04, 2024 23:01Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) hakuwa tu shakhsia wa kidini na kitaifa wa Iran, lakini pia alikuwa nembo ya umma wa Kiislamu.
-
Waziri wa Mambo ya Ndani: Iran itatoa jibu kali na la haraka kwa mashambulizi ya kigaidi ya Kerman
Jan 04, 2024 03:04Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema kuwa vikosi vya usalama na ulinzi vya nchi hii vitatoa jibu la haraka na kali kwa wahusika wa mashambulizi ya kigaidi yaliyoua watu zaidi ya 100 katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.
-
Kuongezeka uwepo wa wanamaji wa Iran katika Bahari Nyekundu
Jan 03, 2024 08:31Meli ya kivita ya Alborz imerudi tena katika Bahari Nyekundu ikiwa ni katika Meli za Kikosi cha 94 cha Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kupitia Lango-Bahari la Bab al-Mandab. Manowari hiyo ya Alborz ilijiunga na Meli za Kusini za Jeshi la Wanamaji Desemba 2019 baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na kuwekwa humo mifumo mipya ya kiteknolojia.
-
Kiongozi Muadhamu: Mkakati mkuu wa Iran ni kutegemea nguvu laini
Jan 03, 2024 08:16Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mkakati mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi hiki cha miaka 45 iliyopita ni kutegemea nguvu laini na nguvu hizo zinapaswa zifanywe kubwa zaidi.
-
Amir-Abdollahian: Jinai za utawala wa Kizayuni zimepiga kengele ya hatari katika ukanda huu mzima
Jan 03, 2024 07:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, jinai na mauaji ya kigaidi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni nje ya mipaka ya Palestina ni tishio kwa usalama na ni kengele ya hatari kwa amani ya ukanda huu mzima.
-
Iran yaipongeza Ansarullah ya Yemen kwa kuiunga mkono Palestina
Jan 02, 2024 03:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameisifu na kuipongeza Harakati ya Ansarullah ya Yemen kwa kuwa na msimamo madhubuti katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.
-
Jenerali Salami: Kinachojiri Gaza ni mauaji ya halaiki
Jan 01, 2024 08:25Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) sanjari na kulaani jinai za kutisha za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa, "Kinachojiri Gaza ni mauaji ya halaiki."