-
Sababu za kuongezeka mashambulio ya kigaidi ya ISIS nchini Iraq
Jan 25, 2021 20:08Jana Jumatatu, Januari 25, 2021, Brigedia Jenerali Yahya Rasoul, msemaji wa Komandi Kuu ya Majeshi ya Iraq alizungumzia ushahidi mpya uliopatikana kuhusu mashambulio ya hivi karibuni ya mjini Baghdad na kusema kuwa, hadi hivi sasa vikosi vya usalama vya Iraq vimefanikiwa kuzima majaribio kadhaa makubwa ya kujiripua kwa mabomu katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
-
Marekani, Saudia na Israel zinachochea hujuma za kigaidi Iraq
Jan 25, 2021 04:20Harakati ya Kata'ib Hizbullah ya Iraq imesema hujuma za kigaidi ambazo zimetekelezwa na kundi la kigaidi la ISIS nchini humo zinachochewa na muungano wa Marekani, Saudi Arabia na Israel.
-
Hatua kali za kiusalama zachukuliwa katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad
Jan 24, 2021 23:01Duru moja ya Iraq imetangaza habari ya kuchukuliwa hatua kali za kiusalama katika mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad hasa baada ya magaidi wa Daesh kufanya mashambulio ya kigaidi yaliyoua na kujeruhi makumi ya watu katikati ya mji huo Alkhamisi iliyopita.
-
Shambulio la DAESH dhidi ya Al-Hashdu-Sha'abi lilifanywa kwa msukumo na msaada wa Marekani
Jan 24, 2021 10:22Chombo kimoja cha habari nchini Iraq kimetangaza kuwa, shambulio la magaidi wa kundi la ukufurishaji la DAESH (ISIS) dhidi ya wapiganaji wa Al-Hashdu-Sha'abi katika mkoa wa Salahuddin limefanywa kwa msukumo na msaada wa Marekani.
-
Waziri Mkuu wa Iraq: Magaidi wa Daesh (ISIS) wasubiri majibu makali ya jinai zao
Jan 22, 2021 08:21Waziri Mkuu wa Iraq amesema kuwa, magaidi wa Daesh (ISIS) wasubiri majibu makali kutoka kwa wananchi na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo na kusisitiza kwamba serikali yake itahakikisha mashambulizi mengine ya kigaidi hayatokei nchini humo.
-
Syria yasisitiza ulazima wa kuweko umoja kwa ajili ya kukabilianan na ugaidi
Jan 22, 2021 04:48Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imelaani mashambulio ya kigaidi yaliyotokea jana katika mji mkuu wa Iraq Baghdad na kusisitiza ulazima wa kuweko umoja na mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya kupambana na ugaidi.
-
Miripuko Iraq, muungano wa "Daulat al Qanun" wataka kuangaliwa upya mikakati ya ulinzi Iraq
Jan 22, 2021 00:25Muungano wa "Daulat al Qanun" umelaani vikali miripuko ya kigaidi iliyotokea jana katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad na kutaka kuangaliwa upya mipango na mikakati ya kulinda usalama wa maeneo yote ya nchi hiyo.
-
Radiamali na sababu za pendekezo la kuakhirishwa uchaguzi wa bunge nchini Iraq
Jan 20, 2021 05:50Tume ya Uchaguzi nchini Iraq imetaka kuakhirishwa kwa miezi minne uchaguzi wa bunge wa nchi hiyo na badala ya kufanyika mwezi Juni, uitishwe mwezi Oktoba mwaka huu wa 2021.
-
Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi: Askari wa Marekani lazima waondoke Iraq
Jan 18, 2021 01:17Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq amesisitiza ulazima wa kutekelezwa mpango uliopitishwa na bunge wa kutaka askari wa jeshi la Marekani waondoke nchini humo.
-
Ujumbe na malengo ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Falih al-Fayadh
Jan 11, 2021 23:02Wizara ya Fedha ya Marekani, siku ya Ijumaa iliweka jina la Falih al-Fayadh, Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya al-Hashd al-Shaabi ya nchini Iraq katika orodha yake ya vikwazo kwa kisingizio cha kukiuka haki za binadamu. Hatua hiyo ya Marekani ina ujumbe muhimu kwa mitazamo kadhaa.