-
Jenerali wa Marekani: Iran ina mbinu nyingi na hatari sana za kupambana na Marekani
Jan 04, 2020 17:05Barry McCaffrey, Jenerali wa Zamani wa Jeshi la Marekani amekiri kwamba Wairan wana mbinu nyingi na hatari sana za kijeshi kwa ajili ya kupambana na Marekani.
-
Kamisheni ya Bunge: Marekani itarajie kisasi kikali kwa hatua yake ya kumuua Qassim Soleimani
Jan 04, 2020 13:14Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni katika Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa, Marekani mtenda jinai isubirie kisasi kikali dhidi yake kutokana na hatua yake ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH).
-
Umati mkubwa wausindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani mjini Baghdad
Jan 04, 2020 12:42Umati mkubwa wa watu umejitokeza leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad kushiriki shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH), aliyeuawa shahidi usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.
-
Kutapatapa viongozi wa Marekani ili kuhalalisha jinai yao ya kumuua shahidi kamanda Soleimani
Jan 04, 2020 11:43Viongozi wa ngazi ya juu wa Marekani wamedhihirisha misimamo ya kukinzana katika juhudi za kuhalalisha jinai yao ya kumuua kigaidi Kamanda Qassem Soleimani baada ya kudai kuwa eti hawataki vita na Iran.
-
Rouhani: Jina la Qassem Soleimani litabakia milele katika historia ya taifa la Iran na wapigania uhuru duniani
Jan 04, 2020 08:16Rais Hassan Rouhani amesema: Jina la Luteni Jenerali Qassem Soleimani litaheshimika na kubakia milele katika historia ya taifa la Iran na wapigania uhuru duniani.
-
Trump akiri hatua ya kigaidi aliyochukua ya kuamuru kuuliwa shahidi Jenerali Soleimani
Jan 04, 2020 07:46Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kuhusu hatua ya kijinai aliyochukua ya kuamuru kutekelezwa operesheni ya mauaji ya kigaidi dhidi ya kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC).
-
Wapalestina: Sehemu kubwa ya juhudi za Shahidi Soleimani zilihusu ukombozi wa Palestina
Jan 04, 2020 07:45Brigedi za shahidi Izzuddin-al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alielekeza sehemu kubwa ya juhudi zake kwa ajili ya kuutokomeza na kuuangamiza utawala wa Kizayuni na kuhitimisha kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Kumuua shahidi Kamanda Soleimani, kosa kubwa mno la kiistratijia la Marekani
Jan 04, 2020 07:36Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa tamko maalumu kufuatia jinai ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH. Taarifa hiyo ya jana Ijumaa ilitolewa baada ya kikao cha dharura cha baraza hilo ambacho kilichunguza pembe mbalimbali za tukio hilo la kuchukua maamuzi yanayofaa.
-
Balozi wa Iran UN: Jibu la mauaji ya kigaidi ya Jenerali Soleimani litakuwa la hatua ya kijeshi
Jan 04, 2020 07:16Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, jibu la mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani yaliyofanywa na Marekani bila shaka litakuwa la hatua ya kijeshi.
-
Mji mkuu wa Nigeria washuhudia mandamano ya kulaani kuuliwa kigaidi Jenerali Soleimani
Jan 04, 2020 03:18Wakazi wa mji mkuu wa Nigeria, Abuja wamefanya maandamanao ya kulaani jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Meja Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH wakati akiwa safarini nchini Iraq.