-
Kushadidi mivutano baina ya Marekani na Ufaransa, Paris yamwita nyumbani balozi wake mjini Washington
Sep 18, 2021 21:52Ufaransa imechukua uamuzi wa kumwita nyumbani balozi wake mjini Washington sambamba na kushadidi mivutano katika uhusiano wa serikali ya Paris na Marekani. Vilevile imechukua hatua ya kumrejesha nyumbani balozi wake nchini Australia kama hatua ya kuonesha malalamiko yake.
-
New York Times: Hizbullah imeishinda na kutoa pigo kwa Marekani
Sep 17, 2021 22:37Gazeti la New York Times la Marekani limekiri kuwa harakati ya Hizzbullah ya Lebanon imeibuka na ushindi katika mpambano wake na Marekani.
-
Nusu ya wanunuzi wa silaha nchini Marekani ni wanawake
Sep 17, 2021 02:57Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa nchini Marekani yanaonyesha kuwa tangu mwaka 2019 hadi mwezi Aprili mwaka huu wanawake wameunda karibu ya nusu ya wamiliki wapya wa silaha nchini humo.
-
Waziri wa Lebanon: Mafuta ya Iran yamevunja vikwazo vya kidhalimu vya Marekani
Sep 16, 2021 07:47Waziri wa Kazi wa serikali mpya ya Lebanon amesema sambamba na kuingia misafara ya mafuta ya Iran katika ardhi ya nchi hiyo kwamba, shehena hizo za mafuta zimevunja mzingiro wa kihistoria na wa kidhalimu ambao Marekani ilikuwa imeiwekea Lebanon.
-
Faida kubwa ya mashirika ya kutengeneza silaha ya Marekani kutokana na tukio la Septemba 11
Sep 15, 2021 21:53Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la Watson Institute for International and Public Affairs la Chuo Kikuu cha Brown nchini Marekani, nusu ya bejeti ya wizara ya ulinzi ya nchi hiyo, Pentagon baina ya miaka ya 2001 hadi 2020 ambayo inafikia dola trilioni 14 imewaendea wakandarasi na mashirika yanayotenegeneza silaha ya nchi hiyo. Kati ya fedha hizo dola trilioni 4.4 zilitengewa vituo vya kijeshi na viwanda vinavyohusika na masuala ya kijeshi.
-
Gazeti la Russia: Iran imefelisha njama za Marekani katika Bodi ya Magavana ya IAEA
Sep 15, 2021 01:54Gazeti la Kommersant la Russia limeandika kuwa, Iran imefelisha njama za Marekani na waitifaki wake wa Ulaya za kutaka kutoa azimio dhidi ya Tehran katika kikao cha Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Zakharova: Lengo la Marekani huko Ukraine ni kuishinikiza Russia
Sep 14, 2021 10:31Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa lengo la mpango wa Marekani eti wa kuimarisha demokrasia nchi ya Ukraine ni kuiweka chini ya mashinikizo Russia na kuyumbisha hali ya mambo katika eneo hilo.
-
Trump: Hakuna njia nyingine isipokuwa mimi nigombee urais mwaka 2024
Sep 14, 2021 02:47Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema alipoulizwa kama atagombea urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2024 au la kwamba, hakuna njia nyingine isipokuwa hiyo.
-
Kukiri Biden kushindwa Marekani kukabiliana na al Qaida; kufeli vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi
Sep 13, 2021 07:37Rais wa Marekani, Joe Biden, siku ya Jumamosi na pembeni mwa sherehe za mwaka wa 20 wa tangu kutokea mashambulio ya Septemba 11 nchini Marekani, alikiri kwamba yumkini kundi la kigaidi la al Qaida likarejea tena Afghanistan na kusisitiza kuwa, Washington haiwezi kupeleka wanajeshi kila sehemu ilipo al Qaida.
-
Kubadilika siasa za nje za Saudia kuhusu uhusiano na madola makubwa
Sep 12, 2021 21:56Hatua ya Saudi Arabia kufutilia mbali safari ya waziri wa ulinzi wa Marekani na wakati huo huo kumkaribisha mjini Riyadh mkuu wa Kamati ya Uhusiano wa Kigeni ya Bunge la Russia Duma, ni jambo linaloashiria kwamba Saudia imeamua kuimarisha uhusiano wake na madola mengine yenye nguvu duniani.