-
Naeem Qassem: Shehena za meli za mafuta za Iran ni mafanikio makubwa ya kisiasa dhidi ya dhulma za Marekani
Sep 11, 2021 21:45Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa shehena za meli za mafuta za Iran zilizotumwa Lebanon kwa ajili ya kupunguza mzingiro wa Marekani dhidi ya nchi hiyo ni mafanikio ya kisiasa na kijamii mbele ya dhulma za serikali ya Washington na jinai zake dhidi ya wanadamu.
-
Mwaka wa 20 tangu baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001
Sep 11, 2021 05:09Jana ikiwa imebakia siku moja kabla ya kutimia mwaka wa 20 tangu baada ya mashambulizi ya Septemba 11 ambayo yaliua watu karibu elfu tatu, Rais Joe Biden wa Marekani alitoa ujumbe akitaka kuwepo umoja na mshikamano wa kitaifa nchini Marekani.
-
Januari 31 yatangazwa kuwa siku ya mwisho ya askari wa Marekani kuwepo katika ardhi ya Iraq
Sep 10, 2021 08:20Kamandi Kuu ya operesheni za pamoja za jeshi la Iraq imetangaza tarehe ya mwisho kwa askari wa jeshi la Marekani kuwepo katika ardhi ya nchi hiyo.
-
Chomsky: Vita vya Marekani dhidi ya 'ugaidi' vimesababisha uharibifu duniani
Sep 09, 2021 22:17Mwanafalsafa na mwanahistoria mashuhuri wa Marekani amesema vita vilivyoanzishwa na Washington miaka 20 iliyopita kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi vimesababisha uharibifu katika sehemu kubwa ya dunia.
-
Al Khazali: Muqawama unasubiri kuondoka kivitendo Marekani
Sep 07, 2021 06:57Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya nchini Iraq amesisitiza kuwa, kamati ya Kuratibu Muqawama inasubiri kuondoka Marekani kivitendo nchini humo.
-
Bloomberg: Nchi tajiri zina dozi ziada zaidi ya bilioni moja za chanjo ya COVID-19
Sep 06, 2021 20:52Shirika la Bloomberg limeripoti kuwa nchi tajiri duniani zina dozi za ziada za chanjo ya COVID-19 zaidi ya bilioni moja licha ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutahadharisha mara kadhaa kuhusu ulimbikizaji wa chanjo hizo.
-
Ubunifu wa Hizbullah na kushindwa siasa za mzingiro na uingiliaji za Marekani
Sep 06, 2021 01:55Ubunifu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon katika kuingiza nchini mafuta kutoka Iran na hivyo kudhibiti mgogoro wa nishati wa nchi hiyo, kunachukuliwa kuwa ishara ya wazi ya kushindwa siasa za mzingiro za Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Onyo la Putin kwa Marekani kwa kuweka mifumo ya makombora katika mpaka wa Russia na Japan
Sep 05, 2021 22:30Rais Vladimir Putin wa Russia ameelezea wasiwasi wake kuhusu mpango wa Marekani wa kuweka mifumo yake ya kujilinda kwa makombora katika mpaka wa Russia na Japan na ameitaka Tokyo isiruhusu kufanyika jambo hilo.
-
Mashinikizo yazidi, Biden aamuru kuchapishwa nyaraka za tukio la Septemba 11
Sep 04, 2021 22:21Rais Joe Biden wa Marekani ametoa taarifa akiamuru kuchunguzwa nyaraka zinazohusiana na tukio la Septemba 11 mwaka 2001 kwa ajili ya kuondolewa nyaraka hizo katika hali ya usiri.
-
Kimbunga Ida chaua watu 61 Marekani, maelfu wapoteza makazi yao
Sep 03, 2021 21:55Kimbunga cha Ida kilichotokea katika majimbo kadhaa ya kaskazini mashariki mwa Marekani kimeua makumi ya watu na kuwafanya maelfu ya wengine wapoteze makazi yao.