-
Tathmini kuhusu hatua ya Marekani kuondoka katika vituo vyake vitatu vya kijeshi Syria
Sep 03, 2021 07:15Marekani imeondoka katika vituo vyake vitatu vya kijeshi vilivyoko katika mikoa ya Deir ez-Zor na Al-Hasakah nchini Syria.
-
Mkuu mpya wa Shin Bet ya Israel aliongoza mauaji ya kamanda wa tawi la kijeshi la HAMAS
Sep 02, 2021 21:57Kwa mara ya kwanza, gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot limetoa taarifa kuhusu mkuu mpya wa shirika la usalama wa ndani la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Shin Bet na kueleza kuwa, afisa huyo ndiye aliyeongoza mauaji ya kigaidi ya mwaka 2012 ya kamanda mwandamizi wa Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya HAMAS ya Palestina.
-
Mufti wa Lebanon: Hizbullah imetuletea fakhari; Marekani ni gonjwa la saratani la Lebanon
Sep 02, 2021 02:59Mufti wa Waislamu wa Kishia nchini Lebanon amesema kuwa, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ni fahari kwa Lebanon na kwamba, kama kuna saratani nchini humo na ulimwenguni, basi saratani hiyo ni Marekani na wafuasi wake.
-
Sisitizo la Biden la kufikia tamati enzi za Marekani za "Ujengaji Taifa kwa operesheni za kijeshi"
Sep 01, 2021 22:28Siku ya Jumanne ya tarehe 31 Agosti, Rais Joe Biden wa Marekani alitoa hotuba maalum kwa mnasaba wa kuondoka rasmi askari wa nchi hiyo katika ardhi ya Afghanistan, ambapo alikufananisha kuondoka katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita kuwa ni sawa na kufikia tamati enzi za kutumia operesheni za kijeshi kwa ajili ya kuzijenga nchi upya; na akasema:
-
Kambi ya kijeshi ya Marekani yashambuliwa kwa maroketi Deir ez-Zor
Sep 01, 2021 02:51Duru za kiusalama zimeripoti habari ya kushambuliwa kwa maroketi kambi ya kijeshi ya Marekani katika mkoa wa Deir ez-Zor, mashariki mwa Syria.
-
Iran yaionya Marekani; Msithubutu kuzuia meli zetu za mafuta zinazoelekea Lebanon
Aug 30, 2021 07:01Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Marekani haina haki wala mamlaka ya kuzuia biashara halali baina ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi nyinginezo duniani huku akiionya vikali Washington dhidi ya kuzuia meli za mafuta za nchi hii zinazoelekea Lebanon.
-
Askari wa Marekani watuhumiwa kuua raia katika shambulio la Kabul
Aug 29, 2021 21:57Baadhi ya raia wa Afghanistan miongoni mwa makumi ya watu waliopoteza maisha katika mkanyagano na fujo lililotokea nje ya Uwanja wa Ndege wa Kabul nchini Afghanistan baada ya kujiri miripuko ya mabomu Alkhamisi iliyopita, yumkini waliuawa na wanajeshi wa Marekani.
-
Ripoti ya mashirika ya upelelezi ya Marekani kuhusu chanzo cha kirusi cha corona
Aug 28, 2021 22:21Mashirika ya upelelezi na ujasusi ya Marekan Ijumaa ya jana yalitangaza muhtasari wa uchunguzi wake kuhusu chanzo cha kirusi cha corona na ugonjwa wa COVID-19 na kutangaza kuwa, maafisa wa serikali ya China hwakuwa na habari yoyote kuhusu kirusi cha corona kabla ya kusambaa kwake duniani mwishoni mwa mwaka 2019.
-
Marekani yaachana na mpango wa kununua 'Ngao ya Chuma' ya Israel
Aug 27, 2021 03:22Jeshi la Marekani limeachana na mpango wake wa kununua mifumo mingine ya ngao ya makombora ya utawala haramu wa Israel, baada ya kuufanyia majaribio mfumo wa kutungua maroketi na makombora ya mafasa mafupi kutoka Tel Aviv mwanzoni mwa msimu huu wa joto kali; na kupata matokeo yasiyoridhisha.
-
Mbunge Mkristo wa Lebanon: Iran ni rafiki yetu; balozi wa Marekani aache uafriti wa kutukwamisha
Aug 26, 2021 22:06Cesar Maalouf, mbunge wa Kikristo katika bunge la Lebanon amesema, Iran si adui wa Lebanon bali ni nchi rafiki; na adui Mzayuni ndiye adui pekee wa Lebanon.