-
Binti wa Donlad Trump ashutumiwa kwa kufanya utapeli
Dec 05, 2020 21:13Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Washington amesema kuwa, matamshi yaliyotolewa na Ivanka Trump, binti wa rais wa Marekani, Donald Trump akijaribu kumvua baba yake na tuhuma za fedha, ni ya kitapeli.
-
Ombi kwa Biden kwa ajili ya kuhitimisha ushiriki wa Marekani katika vita vya Yemen
Dec 05, 2020 21:13Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zina nafasi muhimu katika vita huko Yemen ambavyo viilanzishwa tangu mwezi Machi mwaka 2015 na muungano vamizi chini ya uongozi wa Saudi Arabia kutokana na hatua yao ya kuzipatia Saudia na Imarati misaada mbalimbali ya kilojistiki, kiintelijensia na kijeshi. Kitendo hicho kimekosolewa vikali na jumuiya mbalimbali za kutetea haki za binadamu.
-
Oman yapinga Ansarullah ya Yemen kuwekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi
Dec 05, 2020 09:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amepinga pendekezo la serikali ya Marekani la kuiweka harakati ya Ansarullah ya Yemen kwenye orodha ya makundi ya kigaidi na kusisitiza kuwa kuiita kundi la kigaidi moja ya pande kuu zinazopigana nchini Yemen hakusaidii kutatua mgogoro wa nchi hiyo.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa vikwazo visivyo vya kibinadamu vya Marekani dhidi ya Iran
Dec 05, 2020 00:50Baada ya kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran mashuhuri kama JCPOA mnamo Mei 2018, Marekani ilianza kutekeleza vikwazo vikali zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kupitia siasa zake za kutoa mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Tehran, na kuendelea kuzidisha taratibu vikwazo hivyo vilivyotajwa kuwa vya kulemaza, hata katika kipindi kigumu zaidi cha kuenea virusi vya corona duniani.
-
Mahakama Marekani: Uchunguzi ufanyike kuhusu hali isiyo ya kibinadamu ya watoto wahajiri nchini humo
Dec 04, 2020 01:06Mahakama moja nchini Marekani imetaka kufanyika uchunguzi kuhusu watoto waliohajiri nchini humo na kisha kutenganishwa na familia zao.
-
Madai ya kukaririwa ya Ulaya kuunga mkono JCPOA; nara tupu zisizofungamana na vitendo
Dec 03, 2020 20:45Licha ya kuwa baada ya kujitoa marekani katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia maarufu kama JCPOA, nchi za Ulaya zimekuwa na utendaji hasi na dhaifu katika kulinda na kutekeleza ahadi zao kuhusu mapatano hayo, lakini zingali zinadai kwamba zinaendelea kuyalinda.
-
Iran yataka mshikamano wa dunia katika kukabiliana na hatua za kimabavu
Dec 03, 2020 01:08Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa mjini Vienna, Austria ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwa na mshikamano katika kukabiliana na hatua za kimabavu za upande mmoja.
-
Rais Rouhani: Marekani haina budi kusalimu amri mbele ya muqawama wa taifa la Iran
Dec 02, 2020 07:40Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kushindwa 'siasa za Marekani za mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa' ni jambo ambalo linaifanya serikali mpya ijayo nchini humo isiwe na budi ila kusalimu amri mbele ya muqawama na kusimama kidete taifa hili la Kiislamu.
-
Mauaji ya kiuoga ya mwanasayansi wa Iran na wajibu wa taasisi za kimataifa
Nov 30, 2020 01:05Ikiwa ni katika kudumisha hatua zake za kijinai na kigaidi dhidi ya taifa la Iran, Ijumaa tarehe 27 Novemba utawala wa Kizayuni wa Israel ulitekeleza mauaji mengine ya kigaidi dhidi ya Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi bora na mashuhuri wa Iran, katika mji wa Abesard, mkoani Tehran.
-
Zakharova: Safari ya Pompeo katika miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu huko Syria ni upuuzaji wa sheria za kimataifa
Nov 28, 2020 01:13Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameitaja safari ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani katika miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu huko Syria kuwa ni ishara ya hatua za upuuzaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na Washington.