-
Harakati ya PFLP yataka kutimuliwa Imarati katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
Sep 05, 2020 21:56Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) amesema kuwa, hatua ya Imarati ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel inakinzana na uamuzi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu hivyo ametoa wito wa kutimuliwa nchi hiyo sambamba na kurejeshwa Syria katika jumuiya hiyo.
-
Iran yakaribisha mkutano wa makundi ya Wapalestina huko Beirut
Sep 05, 2020 06:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kikao cha pamoja cha makundi ya Wapalestina kilichofanyika katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut ni ishara kwamba viongozi wa Palestina wapo macho na wamesimama kidete mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na washirika wake.
-
Kikao cha kiistratijia cha Beirut, sauti moja ya Wapalestina
Sep 05, 2020 01:53Makundi ya Palestina yameitisha kikao cha pamoja mjini Beirut, Lebanon na kulaani njama mbalimbali zinazofanywa dhidi ya Palestina na wamesisitiza kuwa kitu kimoja na kuendelea na muqawama katika kukabiliana na njama za Kiarabu/Kimagharibi na Kizayuni.
-
HAMAS yasisitizia umoja wa Wapalestina mkabala wa njama za Israel-Marekani
Sep 04, 2020 02:37Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniya kwa mara nyingine tena amesisitiza udharura wa kuungana na kushirikiana makundi yote ya kisiasa na kijamii ya Palestina kwa lengo kuzima njama za maadui zao, yaani utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na baadhi ya tawala za kizandiki za Kiarabu.
-
Ripota Maalumu wa UN katika masuala ya Palestina aukosoa vikali utawala wa Kizayuni
Sep 03, 2020 06:23Ripota Maalumu na Mtaalamu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Palestina amekosoa vikali hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuuzingira Ukanda wa Ghaza.
-
Arab League yawaacha mkono Wapalestina na kuunga mkono mapatano ya UAE na Wazayuni
Sep 03, 2020 03:38Katika hatua inayoonyesha kuipiga vita na kuiacha mkono Palestina na badala yake kuunga mkono hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya kufanya mapatano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imelikataa ombi la Palestina la kuitishwa kikao cha dharura cha jumuiya hiyo.
-
Malengo ya safari ya Ismail Haniya nchini Lebanon baada ya kupita miaka 27
Sep 03, 2020 02:14Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, baada ya miaka 27 juzi Septemba Mosi aliwasili Beirut mji mkuu wa Lebanon.
-
Harakati ya Kiislamu ya Palestina yakosoa kuanzishwa uhusiano kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni
Aug 31, 2020 02:18Naibu Mkuu wa harakati ya Kiislamu ya Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu amekosoa hatua ya Imarati ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni na kusema: kile kinachotekelezwa na Imarati kwa uungaji mkono wa Saudi Arabia ni vita vya waziwazi dhidi ya imani ya Waislamu.
-
Ismail Haniya: Azma ya muqawama Palestina ni kuhitimisha mzingiro dhidi ya Gaza
Aug 30, 2020 22:05Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, azama na irada ya taifa na muqawama wa Palestina ni kufanya hima kwa ajili ya kuhitimisha mzingiro wa kidhulma unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Nasrullah: Kuanzisha uhusiano na Israel ni huduma ya bwerere kwa Netanyahu na Trump
Aug 30, 2020 22:04Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amekosoa vikali hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kubainisha kuwa: Kitendo hicho cha Abu Dhabi ni huduma bila malipo kwa watawala wa Marekani na Israel wanaoadamwa na misukosuko ya kisiasa.