-
HAMAS: Netanyahu anataka kurefusha vita vya Gaza kwa malengo ya kisiasa
Jan 28, 2024 23:34Mwanachama mwandamizi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kundi hilo la muqawama linataka usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza, lakini Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu anataka vita hivyo viendelee kutokana na sababu zake binafsi na za kisiasa.
-
Umoja wa Afrika wapongeza amri ya ICJ ya kutaka kuzuiwa mauaji ya kimbari Gaza
Jan 28, 2024 10:04Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amekaribisha na kupongeza uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuitaka Israel ichukue hatua zote zinazohitajika kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Maelfu waandamana Madrid kuliunga mkono taifa la Palestina
Jan 28, 2024 09:58Maelfu ya wananchi wa Uhispania kwa mara nyingine tena wamemiminika katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo, Madrid kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina hasa wa Ukanda wa Gaza, na vilevile kulaani mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala haramu wa Israel katika ukanda huo.
-
Wapalestina walaani hatua ya mataifa ya Magharibi ya kusimamisha misaada ya fedha kwa UNRWA
Jan 28, 2024 04:02Maafisa waandamizi wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wamekosoa uamuzi wa karibu nchi kumi za Magharibi wa kusitisha misaada ya fedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada kwa Wapalestina UNRWA na kuzitaka nchi hizo zibadilishe haraka uamuzi wao huo ambao wamesema utasababisha hatari "kubwa".
-
Mahakama ya ICJ yaionya Israel na kuitaka iache kufanya mauaji ya kimbari Gaza
Jan 26, 2024 23:09Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeiamuru Israel iache vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, na kuchukua hatua za kuwasaidia raia.
-
Mbunge Muislamu wa Uingereza amkosoa Waziri Mkuu wa nchi hiyo
Jan 25, 2024 23:48Mbunge Muislamu katika bunge la Uingereza wa chama cha Labour amemkosoa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kuitaja serikali ya London kuwa inabeba dhima ya damu ya maelfu ya Wapalestina wasio na hatia.
-
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Poland waandamana kupinga uungaji mkono wa Ujerumani kwa Israel
Jan 25, 2024 23:48Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Warsaw nchini Polanda wameandamana kupinga uungaji mkono wa serikali ya Ujerumani kwa utawala wa Kizayuni.
-
Seneta Sanders: Washington ni mshirika wa jinai za Israel huko Gaza
Jan 25, 2024 08:12Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani amesema serikali ya Washington ni mshirika katika jinai za kutisha za Israel huko Ukanda wa Gaza kutokana na uungaji mkono wake kwa utawala huo unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Palestina: Kwa siku 108, Israel imeua watoto 11,000 na wanawake 7,500 Gaza
Jan 23, 2024 03:08Mamlaka za Palestina zimetangaza kuwa, jeshi vamizi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeua watoto 11,000 na wanawake 7,500 katika Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa jeshi hilo katili limedondosha zaidi ya tani 65,000 za mada za miripuko katika vita vya upande mmoja lilivyoanzisha dhidi ya Wapalestina waliowekewa mzingiro.
-
Misri yaionya Israel kutoudhibiti Ukanda wa Philadelphi kwenye mpaka wa Palestina
Jan 23, 2024 02:04Misri imeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba jaribio lolote la kuikalia kwa mabavu sehemu ya ardhi inayotenganisha eneo la Wapalestina lililozingirwa la Ukanda wa Gaza na Misri, linalojulikana kama Korido ya Philadelphi, litakuwa ni "tishio kubwa" kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili.