Pars Today
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA, Yukia Amano, amewasili Tehran leo asubuhi na kufanya mazungumzo na mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Ali Akbar Salehi.
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema Marekani inaendelea kukiuka mapatano ya nyuklia ya Iran na madola sita makubwa duniani.
Iran itachukua hatua kali na imara iwapo kutakuwepo ukiukwaji wowote wa mapatano ya nyuklia baina yake na madola sita makubwa duniani.
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema karibuni dawamiale (Radiopharmaceuticals) zinazotengezwa nchini zitaanza kusafirishwa na kuuzwa kwa wingi nje ya nchi.
Makamu wa Rais wa Iran, ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki amesema uchumi wa taifa hili unategemea uwezo wa ndani na unaelekea kwenye kilele cha ustawi.
Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, Tehran imeamua kutoitumia tena Marekani maji mazito ya nyuklia.