-
Hamas yawapongeza mabalozi wa zamani wa Ufaransa na Uingereza wanaotaka Israel iwekewe vikwazo
Aug 23, 2026 13:57Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imepongeza muungano wa wanadiplomasia zaidi ya 100 wa zamani wa Ufaransa na Uingereza wanaozitaka serikali za nchi zao kushirikiana kulinda sheria za kimataifa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina. Mabalozi hao pia wametaka Israel iwekewe vikwazo.
-
Iran yawatimua wanadiplomasia wawili wa Ufaransa kutokana na mienendo yao haramu
Aug 19, 2026 10:05Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imewatangaza wanadiplomasia wawili wa Ufaransa wanaofanya kazi katika Ubalozi wa Ufaransa mjini Tehran kuwa ni watu wasiostahili kutokana na shughuli zao zinazotambuliwa kuwa kinyume na sheria za kimataifa na Mkataba wa Vienna wa 1961 kuhusu Mahusiano ya Kidiplomasia.
-
Lavrov: Wanajeshi wa Ukraine Wanahusika na Ugaidi dhidi ya Nchi za Afrika
Aug 18, 2026 11:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, amesema kuwa Moscow imetiwa wasiwasi na ripoti zinazoashiria kuwa wanajeshi wa Ukraine wanahusika katika operesheni zinazotekelezwa na makundi haramu ya wanamgambo dhidi ya nchi za ukanda wa Sahel barani Afrika.
-
Rais wa Burkina Faso atoa tamko kuhusu mivutano ya madaraka nchini humo
Jul 23, 2026 11:47Rais wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traore, ametoa kauli nzito inayolenga kukomesha uvumi wa kuwepo kwa mivutano ya madaraka ndani ya safu za uongozi wake, akisisitiza dhamira yake ya kusalia kama kiongozi mkuu pekee wa taifa hilo. Traore aliwaambia viongozi wa jamii hivi karibuni mjini Ouahigouya, kaskazini mwa nchi hiyo kwamba: “Meli haiwezi kuwa na manahodha wawili,”
-
Tel Aviv inawakera hata washirika wake, Ufaransa yalituhumu shirika la Israel kuingia mambo ya ndani ya nchi hiyo
Jun 16, 2026 02:52Baada ya takriban mwezi mmoja wa uchunguzi rasmi, Paris imeituhumu kampuni ya Israel kwa kuingilia uchaguzi uliopita nchini Ufaransa, na imetaka maelezo kutoka Tel Aviv kuhusu suala hilo.
-
Mkaguzi mkuu wa magereza Ufaransa: Hali ya magereza nchini ni "mbaya, ya aibu na ya majanga"
Jun 01, 2026 02:39Wizara ya Sheria ya Ufaransa imetangaza kwamba idadi ya wafungwa nchini humo imefikia zaidi ya watu 88,600, ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika historia ya nchi hiyo.
-
Rais Macron akabiliwa na upinzani baada ya matamshi yake makali kwenye mkutano wa Nairobi
May 13, 2026 12:14Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anakabiliwa na upinzani mkali baada ya kukatiza kikao cha mjadala katika kongamano la Africa Forward Summit nchini Kenya akiwataka hadhirina wanyamaze kimya.
-
Kenya yataka Afrika ipewe kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la UN
May 12, 2026 14:25Rais wa Kenya, William Ruto, ametoa wito kwa Afrika kupewa uanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, takwa ambalo limeungwa mkono na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
-
Pezeshkian amwambia Macron: Iran yataka diplomasia huku ikisisitiza kulinda haki za taifa
May 07, 2026 08:07Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amemwambia mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kuwa Tehran iko tayari kuendelea kwa dhati na njia za kidiplomasia ili kukomesha vita, huku ikisisitiza umuhimu wa kulindwa haki za taifa la Iran.
-
Rais wa Iran amwambia Macron: US, Israel ndio mzizi wa ukosefu wa usalama katika eneo
Mar 16, 2026 06:04Rais wa Iran amesema Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ndizo chimbuko la ukosefu wa usalama na uthabiti katika eneo la Asia Magharibi, akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitasita kukabiliana na wavamizi.