-
Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah aaga dunia
Mar 20, 2022 08:40Spika wa Bunge la Kitaifa la Uganda, Jacob L'Okori Oulanyah amefariki dunia akitibiwa nchini Marekani.
-
Jeshi la Uganda limekanusha kuwa mtoto wa Museveni amejiuzulu
Mar 14, 2022 10:25Jeshi la Uganda limesema leo Jumatatu kwamba mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye anatajwa kuwa ndiye atakayerithi miikoba ya baba yake kama rais ajaye wa Uganda, hajajiuzulu.
-
ICJ yaiamuru Uganda kuilipa DRC dola milioni 325 tu kufidia gharama za vita
Feb 10, 2022 04:05Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imetangaza kuwa dola milioni 325 ndio kiasi cha fidia ambacho Uganda inapaswa kuilipa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ilikuwa ikidai zaidi ya dola bilioni 11 kwa uvamizi uliofanywa na jeshi la serikali ya Kampala mashariki mwa nchi hiyo wakati wa vita vya miaka ya 1998-2003.
-
Watanzania 3 wakamatwa DRC wakituhumiwa kuwa wanachama wa ADF
Feb 08, 2022 04:16Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza habari ya kuwatia mbaroni raia watatu wa Tanzania, kwa tuhuma za kuwa wanachama wa kundi la wanamgambo wa ADF.
-
Viongozi wa Kiislamu Uganda waunga mkono serikali kuhusu mwaka mpya + Sauti
Jan 02, 2022 03:22Serikali ya Uganda imepiga marufuku mijumuiko ya kusherehekea mwaka mpya ili kuzuia maambukizi ya Corona hatua ambayo imeungwa mkono na viongozi wa Kiislamu
-
Rais Museveni asema shule zitafunguliwa Uganda mwezi huu
Jan 01, 2022 09:08Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kuwa, shule za nchi hiyo ambazo zilikuwa zimefungwa tokea Machi 2020 kutokana na msambao wa maradhi ya Covid-19, sasa zitafunguliwa mwezi huu wa Januari, 2022.
-
DRC: Jeshi la Uganda ladai kutwaa moja ya kambi kuu za ADF + SAUTI
Dec 29, 2021 08:43Jeshi la Uganda linasema limefanikiwa kudhibiti kambi kubwa ya waasi wa ADF, inayofahamika kama Kambi Ya Yua iliyokuwa inawahifadhi waasi zaidi ya 600 na familia zao, katika operesheni zao inazoshirikiana na wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mashariki mwa nchi hiyo.
-
Wananchi wa Uganda walalamikia kutoona matunda yoyote ya Uhuru + SAUTI
Dec 29, 2021 05:21Tangu mkoloni Muingereza aondoke Uganda miaka 59 iliyopita raia wa nchi hiyo hawajaona faida yoyote katika maisha yao ya kila siku
-
Washukiwa watano wa miripuko ya kigaidi Uganda wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi
Nov 19, 2021 08:25Polisi ya Uganda imesema, imewaua kwa kuwapiga risasi washukiwa watano na kuwatia nguvuni watu 21 kufuatia miripuko pacha ya mashambulio ya mabomu ya siku ya Jumanne iliyopita, ambayo iliua watu wasiopungua watano na kujeruhi makumi ya wengine katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.
-
Askari 2 wa Uganda wahukumiwa kifo kwa mauaji ya raia Somalia
Nov 14, 2021 04:46Askari wawili wa Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) wanaohudumu kwenye Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) wamehukumiwa kifo, kutokana na mauaji ya raia katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.