-
Nchi za Waislamu zataka kuruhusiwa misaada ya kibinadamu Gaza
Jan 03, 2026 02:42Mawaziri wa Mambo ya Nje wa mataifa manane ya Waislamu wameitaka jamii ya kimataifa kuishinikiza Israel, kama dola linalokalia kwa mabavu ardhi za Palestina, kuondoa mara moja vizingiti na vikwazo vya kuingia kwa misaada ya msingi na ya dharura katika Ukanda wa Gaza.
-
Al-Jazeera: Israel inajiandaa kuanzisha tena mashambulizi makali Gaza
Jan 02, 2026 23:07Waziri wa Vita wa Israel, Israel Katz ameliagiza jeshi la utawala huo haramu kujiandaa kurejea kwenye mapigano makali dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza, hayo yameripotiwa na kanali ya televisheni ya al-Jazeera ikinukuu gazeti la Kizayuni la The Jerusalem Post.
-
Israel yakemewa, yalaaniwa kimataifa kwa kupiga marufuku asasi 37 zinazotoa misaada Ghaza
Jan 01, 2026 02:33Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani marekebisho ya sheria yaliyopitishwa na Bunge la utawala wa kizayuni wa Israel, Knesset Desemba 29, yanayohusu kusitishwa shughuli za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).
-
Israel yasitisha shughuli za mashirika ya misaada zaidi ya 30 huko Gaza chini ya sheria mpya za usajili
Dec 31, 2025 22:55Israel imesimamisha shughuli za mashirika ya kimataifa 30 ya masuala ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. Waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu wamekosoa na kulaani vikali hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni.
-
Papa Leo azungumzia madhila ya Wapalestina wa Ghaza katika ibada ya Krismasi
Dec 26, 2025 03:00Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amesema katika mahubiri ya Krismasi aliyotoa jana Alkhamisi kwamba anasikitishwa na madhila yanayowafika Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Abu Hatab wa Ghaza asimulia alivyoshiriki kuzika Wapalestina 18,000 waliouliwa kinyama na Israel
Dec 23, 2025 08:32Mzikamaiti Yousef Abu Hatab mkazi wa Ukanda wa Ghaza na mmoja wa mashuhuda wa moja ya majanga makubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Palestina, amesema ameshiriki kuzika karibu miili 18,000 ya Wapalestina waliouliwa shahidi wakati wa vita vya kinyama na vya mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel katika eneo hilo la Palestina.
-
Wademocrat wataka kushinikizwa Israel kwa kukiuka usitishaji vita Gaza
Dec 23, 2025 04:30Makumi ya Wademokrat katika Bunge la Marekani wameitaka Ikulu ya Rais wa nchi hiyo (White House) kuushinikiza kidiplomasia utawala wa Israel ili usitishe ukiukaji wa mapatano ya kutisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
-
Baridi kali yaua Wapalestina 17 Gaza; Israel yaendelea kuzuia misaada
Dec 18, 2025 06:56Dhoruba na baridi kali zimesababisha vifo vya Wapalestina 17 katika Ukanda wa Gaza tangu mwanzoni mwa mwezi huu, kwa mujibu wa serikali za mitaa Gaza, huku Israel ikishadidisha vikwazo vikali vya kuingia kwa vifaa vya kuunda makazi na misaada mingine ya kibinadamu katika eneo hilo la Palestina lililokumbwa na vita.
-
Qatar: Ukiukaji wa usitishaji mapigano wa Israel 'unahatarisha' mchakato mzima wa Gaza
Dec 18, 2025 06:55Waziri Mkuu wa Qatar ameonya kwamba, ukiukaji unaofanywa kila siku wa Israel wa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza unatishia mchakato mzima wa mapatano hayo, huku akitoa wito wa kutekelezwa haraka awamu inayofuata ya makubaliano hayo ili kukomesha vita vya mauaji ya halaiki vya Israeli dhidi ya eneo la Wapalestina lililozingirwa.
-
Albanese: Israel na waungaji mkono wake wakuu inawapasa wagharamie ujenzi mpya wa Ghaza
Dec 13, 2025 08:06Francesca Albanese, Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu amesema, Israel na Marekani pamoja na nchi zingine ambazo zilikuwa wasambazaji wakuu wa silaha kwa utawala huo, zinapaswa kugharimia ujenzi mpya wa eneo la Ukanda wa Ghaza.