-
UN yaitaka Israel ikomeshe 'mfumo wa ubaguzi wa apathaidi' inaoendesha Ukingo wa Magharibi
Jan 08, 2026 03:05Umoja wa Mataifa kupitia Kamishna wake Mkuu wa Haki za Binadamu umesema, hatua za miongo kadhaa za Israel za kuwatenga na kuwabagua Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi inaoukalia kwa mabavu zinazidi kuongezeka, na kwa sababu hiyo umetoa wito wa kuutaka utawala huo ukomeshe "mfumo wake wa ubaguzi wa rangi wa apathaidi".
-
Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel huko Somaliland; Tel Aviv katika njia ya kuyumbisha amani Pembe ya Afrika
Jan 08, 2026 03:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel amefanya safari huko Hargeisa, mji mkuu wa eneo la Somaliland, akiongoza ujumbe rasmi wa Israel.
-
Imarati inapanga kuijengea Israel kambi ya jeshi karibu na Saudi Arabia
Jan 07, 2026 10:13Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimefichua mpango wa Umoja wa Falme za Kiarabu wa kujenga kambi ya kijeshi ya Israel karibu na mpaka wa nchi hizi mbili za Kiarabu.
-
Hatari za kisiasa na kiusalama za hatua ya utawala wa Israel ya kutambua rasmi Somaliland
Jan 06, 2026 10:34Kufuatia hatua ya utawala wa Israel ya kulitambua rasmi eneo la Somaliland huko Somalia kama nchi huru, kumetolewa maonyo kuhusu matokeo hatari ya kisiasa na kiusalama ya kitendo hicho.
-
Kamanda: Baada ya kushindwa vita vya Juni, US na Israel zinaendesha 'vita laini' kuvuruga utulivu Iran
Jan 05, 2026 03:17Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel zinaendesha "vita laini" ili kuvuruga uthabiti na utulivu nchini likiwa ni jaribio la kufidia kushindwa kwao katika vita vya siku 12 vya mwezi Juni zilivyoanzisha dhidi ya Iran.
-
Al-Jazeera: Israel inajiandaa kuanzisha tena mashambulizi makali Gaza
Jan 03, 2026 02:37Waziri wa Vita wa Israel, Israel Katz ameliagiza jeshi la utawala huo haramu kujiandaa kurejea kwenye mapigano makali dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza, hayo yameripotiwa na kanali ya televisheni ya al-Jazeera ikinukuu gazeti la Kizayuni la The Jerusalem Post.
-
Iran yajibu bwabwaja, vitisho na matamshi ya uingiliaji ya Trump
Jan 02, 2026 10:17Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameonya kwamba, uingiliaji kati wa Marekani katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu utavuruga utulivu wa eneo zima la Asia Magharibi na kuhatarisha moja kwa moja maslahi ya Marekani katika eneo.
-
Baraza la Makanisa Duniani lataka kuwekewa vikwazo Israel kutokana na vita vya Gaza
Jan 02, 2026 02:48Baraza la Makanisa Duniani (WCC) limeutaka Umoja wa Ulaya (EU) kuiwekea Israel vikwazo vikiwemo vya silaha kutokana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza, na ukiukaji wa haki dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
-
Somaliland yajitoa kimasomaso, yakanusha kuafiki kujengwa kambi za kijeshi za Israel
Jan 02, 2026 02:46Eneo la Somaliland la kaskazini mwa Somalia limekanusha madai kwamba lilikubali kuwa mwenyeji wa vituo vya kijeshi vya Israel na kuwapokea Wapalestina waliofurushwa kutoka Gaza ili kutambuliwa na Israel.
-
Kwa nini kiwango cha kujiua katika jeshi la Israel kimefikia kiwango cha juu zaidi?
Jan 02, 2026 02:36Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Isarel, kwa kukiri kujiua kwa makumi ya wanajeshi wake, limekubali kuwa jumla ya wanajeshi 151 wamepoteza maisha katika mwaka huu wa sasa.