-
UN: DRC inakabiliwa na moja ya hali mbaya zaidi za kibinadamu duniani
Aug 23, 2025 06:06Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inakabiliana na mojawapo ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani, huku machafuko na ukosefu wa usalama vikiendelea kuwaangamiza raia mashariki mwa nchi hiyo.
-
Uganda yaafiki kuwapokea wahamiaji waliotimuliwa Marekani kama hawana rekodi za uhalifu
Aug 23, 2025 06:01Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema, nchi hiyo itakubaliana na mpango wa Marekani wa kuwapokea wahamiaji waliofukuzwa nchini humo ikiwa hawatakuwa na rekodi za uhalifu au si watoto wasio na jamaa zao.
-
Mwendesha mashtaka wa DRC ataka Kabila ahukumiwe kifo
Aug 23, 2025 02:45Mwendesha mashtaka wa kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametoa mwito wa kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Joseph Kabila ambaye mashitaka dhidi yake yanaendelea bila ya yeye kuwepo mahakamani.
-
Shambulizi la droni Sudan lateketeza malori 16 ya Umoja wa Mataifa
Aug 23, 2025 00:27Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, shambulizi la droni katika msafara umesababisha kuteketea kwa malori 16 ya misaada iliyokuwa inahitajika mno katika eneo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, lililokumbwa na uhaba mkubwa wa chakula.
-
Viwiliwili visivyopungua vitano vya wahanga wa itikadi kali za kidini vyafukuliwa Kenya
Aug 22, 2025 08:20Viwiliwili visivyopungua vitano vimefukuliwa kutoka kwenye makaburi yenye kina kifupi katika eneo moja la pwani kaskazini ya Kenya, ambako wahanga wa itikadi kali za kidini wanashukiwa kuwa walizikwa.
-
Raia 102 wa kigeni magaidi na matapeli wa mitandaoni watimuliwa Nigeria, wengi wao ni Wachina
Aug 22, 2025 06:34Serikali ya Nigeria imewatimua raia wa kigeni 102 wakiwemo Wachina 50 waliopatikana na hatia ya kuhusika na "ugaidi wa mitandaoni na utapeli wa mitandaoni".
-
Jeshi la Sudan lakanusha kushambulia msafara wa misaada wa WFP katika jimbo la Darfur
Aug 22, 2025 06:33Jeshi la Sudan (SAF) limekanusha madai yaliyotolewa wapiganaji wa Vikosi vya Usaidzi wa Haraka (RSF) kuwa limefanya mashambulizi ya angani dhidi ya msafara wa misaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) uliokuwa unapeleka misaada Darfur.
-
Wabunge wa Kenya wamtaka Rais Ruto awasilishe mahakamani ushahidi wa wabunge kula hongo
Aug 22, 2025 04:01Uongozi wa Bunge la Kitaifa la Kenya umepuuza matamshi yaliyotolewa na Rais William Ruto kuhusu madai ya hongo bungeni, ukisema ni tuhuma tupu, na kumtaka atoe ushahidi wa madai hayo ya ufisadi.
-
Jibu la Tunisia kwa kauli ya Netanyahu ni ishara ya wasiwasi wa nchi za Kiarabu kuhusu mipango ya upanuzi ya Israel
Aug 21, 2025 22:43Wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano ya kupinga uzayuni wakilaani matamshi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, kuhusu kile kinachoitwa “Israeli Kubwa.”
-
Amnesty International: Haki za binadamu zimekiukwa mashariki mwa Kongo
Aug 21, 2025 22:42Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International, limezituhumu pande zinazozozana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kufanya ukiukwaji wa kutisha wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na vitendo vya kubaka kwa umati, mauaji ya kiholela na utekaji nyara.