-
Human Rights Watch yakosoa kitendo cha Burkina Faso kumfukuza afisa wa UN
Aug 21, 2025 08:13Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limekosoa uamuzi wa serikali ya kijeshi ya Burkina Faso kumfukuza mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Carol Flore-Smereczniak, na kumtangaza kuwa "mtu asiyetakikana," nchini humo na kutoa wito kwa mamlaka ya kijeshi kushirikiana na Umoja wa Mataifa badala ya "kuficha ukiukwaji wa haki za binadamu."
-
Makubaliano ya amani ya DRC: Maeneo yanayodhibitiwa na M23 kurejeshwa mikononi mwa serikali
Aug 21, 2025 06:24Makubaliano ya amani yaliyopendekezwa kati ya serikali ya Congo na waasi wa M23 wanaodaiwa kuuungwa mkono na Rwanda yanataka kurejesha udhibiti wa serikali katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi.
-
Makumi waaga dunia kwa mafuriko nchini Niger, maelfu waathirika
Aug 21, 2025 02:12Kwa uchache watu 47 wamepoteza maisha, huku zaidi ya 56,000 wakilazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha hivi majuzi nchini Niger.
-
Amnesty yaikosoa Nigeria kwa kuwakandamiza Waislamu wakiitetea Gaza
Aug 21, 2025 01:43Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International nchini Nigeria, Isa Sunusi, amelaani vikali ukandamizaji mkali wa vyombo vya serikali dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, wakati wa maandamano ya kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza, na kusema kuwa takriban wanachama 83 wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria bado wako rumande bila kufunguliwa mashtaka, licha ya kupata majeraha ya risasi na makovu mengineo wakishiriki maandamano ya amani.
-
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan: Tunafanya kazi kwa bidii kudhibiti usalama na uwepo wa kigeni nchini
Aug 21, 2025 08:14Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan, Luteni Jenerali Babiker Samra amesema kwamba uwepo haramu wa wapiganaji wa kigeni nchini humo hauwezi tena kuvumiliwa, kutokana na athari zake mbaya za kiusalama, kiuchumi na kijamii.
-
Ajali ya boti yaua watu wasiopungua 22 kaskazini magharibi mwa Nigeria
Aug 20, 2025 23:52Watu wasiopungua 22 wanaaminika kuwa wameaga dunia baada ya boti waliyokuwa wameabiri ndani yake kuzama kaskazini magharibi mwa Nigeria. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la huduma za dharura la nchi hiyo.
-
Katibu Mkuu wa UN: Afrika inapasa iwe ya kwanza kunufaika na madini yake muhimu
Aug 20, 2025 23:32Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na Afrika, akisisitiza kwamba nchi zinazoshikilia utajiri mkubwa wa madini wa bara hilo lazima ziwe za kwanza kunufaika.
-
Kwa nini utawala wa kizayuni wa Israel unataka kuzidisha satua na ushawishi wake barani Afrika?
Aug 20, 2025 23:29Katika mwendelezo wa hatua za kujaribu kuwa na satua na ushawishi katika nchi za Kiafrika, waziri wa mambo ya nje wa utawala wa kizayuni wa Israel Gideon Saar siku ya Jumanne alielekea Zambia katika safari ya kidiplomasia barani Afrika, madhumuni makuu yakiwa ni kufungua ubalozi wa utawala huo haramu nchini humo.
-
HRW: Waasi wa M23 wameuwa raia zaidi ya 140 mashariki mwa Kongo
Aug 20, 2025 08:28Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeeleza hii leo kuwa waasi wa kundi la M23 limeuwa raia zaidi ya 140 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje: Uganda haijakubaliana na Marekani kupokea wahamiaji haramu
Aug 20, 2025 08:27Uganda imesema kuwa haijafikia makubaliano na Marekani kuwapokea nchini humo wahamiaji haramu kwa sababu haina miundomsingi inayohitajika kufanya hivyo.