-
Uwanja wa Ndege Khartoum washambuliwa na RSF kabla ya kufunguliwa
Oct 21, 2025 07:29Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vimeripotiwa kushambulia maeneo muhimu katika mji mkuu wa Sudan, ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo.
-
Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Madagascar amteua mfanyabiashara kuwa waziri mkuu mpya
Oct 21, 2025 03:31Rais wa mpito wa Madagascar Kanali Michael Randrianirina amemteua mfanyabiashara Herintsalama Rajaonarivelo kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo na kumuapisha katika hafla rasmi iliyofanyika kwenye Ikulu ya Jimbo la Iavoloha.
-
Ripoti: Mashambulizi ya wanamgambo yameshadidi eneo la Sahel Afrika
Oct 20, 2025 23:28Mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha yanaripotiwa kushadidi katika eneo la Sahel Afrika.
-
Amnesty International: Serikali ya Tanzania imezidisha ukandamizaji kabla ya uchaguzi mkuu
Oct 20, 2025 23:28Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limesema kuwa, serikali ya Tanzania imezidisha ukandamizaji kwa wakosoaji wake wa kisiasa, waandishi wa habari, asasi za kiraia, na watetezi wa haki za binadamu katika juhudi za kudumisha madaraka na kuzuia ushiriki wa raia.
-
Afrika katika makucha ya ukoloni mamboleo, ushindani wa kimataifa kwa ajili ya rasilimali muhimu na vitisho vipya
Oct 20, 2025 12:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amekutana na mwenzake wa Liberia, Sara Beysolow Nyanti kujadili njia za kupanua ushiriki wa Marekani katika sekta muhimu ya madini nchini Liberia.
-
WHO: Mgonjwa wa mwisho wa Ebola Kongo aruhusiwa kutoka katika kituo cha matibabu
Oct 20, 2025 03:12Shirika la Afya Duniani (WHO) jana liliripoti kuwa mgonjwa wa mwisho wa Ebola aliruhusiwa jana kutoka kwenye kituo cha matibabu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Mashujaa Dei kufanyika kama kawaida Kenya licha ya maombolezo ya kifo cha Raila Odinga
Oct 19, 2025 23:52Serikali ya Kenya imetangaza kuwa Siku ya Mashujaa itaadhimishwa leo kama kawaida licha ya hofu iliyokuwepo kwamba ingeahirishwa baada ya kifo cha waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Raila Odinga.
-
Gavana wa Darfur: Mashambulizi ya RSF huko El Fasher ni sawa na mauaji ya halaiki
Oct 19, 2025 23:06Gavana wa Darfur, magharibi mwa Sudan, Minni Arko Minawi, amesema kuwa mashambulizi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) dhidi ya El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, ni sawa na mauaji ya halaiki.
-
Wamisri wataka kufunguliwa tena kivuko cha mpakani na Ukanda wa Gaza
Oct 19, 2025 23:02Huku msaada wa kibinadamu unaohitajika ukisalia kuwa haba huko Gaza, waanchi wa Misri wametaka kufunguliwa tena kivuko cha mpakani cha Rafah kwa ajili ya kuingiza misaada neo la Ukanda wa Gaza.
-
Burhan: Jeshi la Sudan liko tayari kwa mazungumzo ili kurejesha umoja
Oct 19, 2025 07:53Jenerali Abdel-Fattah al Burhan, Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan amesema jeshi la nchi hiyo liko tayari kwa mazungumzo ya "kumaliza vita na kurejesha umoja na heshima ya nchi hiyo."