Afrika
  • ADF yanyooshewa kidole cha lawama kwa mauaji mapya ya Kivu Kaskazini

    ADF yanyooshewa kidole cha lawama kwa mauaji mapya ya Kivu Kaskazini

    Aug 18, 2025 05:01

    Waasi wa ADF wameongeza mashambulizi dhidi ya raia katika siku za hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Jumapili ya jana, Agosti 17, watu wasiopungua tisa waliuawa katika mji wa Oicha, makao makuu ya eneo la Beni, kulingana na vyanzo vya afya na utawala vya eneo hilo.

  • Maandamano ya kutaka kulindwa wanahabari wa Gaza yafanyika Afrika Kusini

    Maandamano ya kutaka kulindwa wanahabari wa Gaza yafanyika Afrika Kusini

    Aug 18, 2025 03:18

    Waandishi wa habari wa Afrika Kusini na wafanyakazi wa vyombo vya habari wameongoza maandamano huko Sea Point jijini Cape Town, wakishinikiza kupewa ulinzi zaidi waandishi wa habari wa Palestina huko Gaza, sanjari na kutangaza mshikamano na wenzao waliouawa katika ukanda huo wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

  • Qatar: Tumezikabidhi DRC, M23 rasimu ya makubaliano ya amani

    Qatar: Tumezikabidhi DRC, M23 rasimu ya makubaliano ya amani

    Aug 18, 2025 03:14

    Qatar imetangaza habari ya kukabidhi rasimu ya makubaliano ya amani kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi la waasi la M23, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa amani unaoendelea Doha, vyombo vya habari vya DRC viliripoti hayo jana Jumapili, vikimnukuu afisa wa Qatar.

  • Wanahabari Nigeria walaani mauaji ya waandishi wenzao huko Gaza

    Wanahabari Nigeria walaani mauaji ya waandishi wenzao huko Gaza

    Aug 18, 2025 03:13

    Muungano wa Waandishi wa Habari wa Nigeria (NUJ) umelaani vikali mauaji ya wanahabari yaliyofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na kusisitiza kuwa, hujuma hizo za utawala wa Kizayuni dhidi ya waandishi wenzao katu haziwezi kuwazuia wahudumu wa tasnia hiyo kuendelea kufichua ukweli.

  • Madaktari wa Sudan: RSF imeua watu wengi kwenye kambi ya Abu Shouk, wamo watoto saba

    Madaktari wa Sudan: RSF imeua watu wengi kwenye kambi ya Abu Shouk, wamo watoto saba

    Aug 17, 2025 23:56

    Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa, wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) wamefyatua makombora kwenye kambi ya wakimbizi waliokumbwa na njaa katika eneo la magharibi mwa Darfur na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 31 wakiwemo watoto saba na mwanamke mjamzito.

  • DRC yapinga kupelekwa balozi mdogo wa Kenya mjini Goma

    DRC yapinga kupelekwa balozi mdogo wa Kenya mjini Goma

    Aug 17, 2025 08:07

    Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepinga hatua ya Kenya ya kumteua balozi mdogo anayetazamiwa kutumwa katika mji wa Goma ulioko mashariki mwa DRC, ikiuelezea uamuzi huo kuwa "usiofaa".

  • Tanzania, Burundi zazindua ujenzi wa reli ya SGR Uvinza-Musongati

    Tanzania, Burundi zazindua ujenzi wa reli ya SGR Uvinza-Musongati

    Aug 17, 2025 00:22

    Mataifa mawili Jirani ya Tanzania na Burundi yamezindua ujenzi wa reli ya SGR Uvinza-Musongati.

  • Ramzy Abou Ibrahim aapa kulitetea taifa lake la Palestina

    Ramzy Abou Ibrahim aapa kulitetea taifa lake la Palestina

    Aug 16, 2025 22:56

    Ramzy Abou Ibrahim, mkuu wa Jumuiya ya Wapalestina nchini Nigeria, amesema kuwa, Wapalestina kamwe hawatasalimisha ardhi yao licha ya uvamizi wa Israel, huku wakitetea kwa dhati haki ya Hizbullah ya kumiliki wa silaha dhidi ya vikosi vinavyokalia kwa mabavu.

  • Kenya yalaumiwa kwa kupuuza ripoti ya dhulma kwa watoto

    Kenya yalaumiwa kwa kupuuza ripoti ya dhulma kwa watoto

    Aug 16, 2025 07:47

    Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International, limemshtumu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen kwa kupuuza uchunguzi uliofanywa na shirika moja kuhusu ulanguzi wa watoto nchini humo.