Mwendesha mashtaka ataka Felicien Kabuga arejeshwe Rwanda
Mwendesha mashitaka wa kitengo cha Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) ametoa ombi la kurejeshwa Rwanda Felicien Kabuga anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Rwanda.
Mwendesha mashitaka wa kitengo cha Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) kilichosalia kusikiliza kesi zilizoachwa na Mahakama hiyo ya Arusha amekitaka kitengo hicho kufanya utafiti wa kuachiwa kwa muda kwa Félicien Kabuga na kuhamishiwa Rwanda, nchi alikozaliwa ambayo "ndio pekee imeonyesha nia ya kumpokea". Hiyo ni kwa mujibu wa waraka kutoka katika kitengo hicho.
Kwa sasa Kabuga anazuiliwa katika gereza la The Hague, Uholanzi, baada ya chumba cha taasisi inayofanya kazi huko mnamo mwezi Septemba, 2024 kuamua kusitisha kwa muda usiojulikana kesi ya Kabuga mwenye umri wa miaka 90 kwa sababu za kiafya, na kwamba ataachiliwa kwa dhamana.
Kabuga alishtakiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kifedha kwa mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda, mashtaka aliyoyaita "uongo".
Sikuu ya Jumanne mjini Arusha, Tanzania, jopo la majaji watatu; Iain Bonomy, Mustapha El Baaj na Margaret M. deGuzman na ripota Bw. Abubacarr M. Tambadou msajiliwa mahakama walijadili kuhusu kuachiliwa kwa muda kwa Kabuga na kurejeshwa Rwanda.
Hati hiyo ya mahakama inasema kwamba kutokana na matukio ya miaka miwili
Baadhi ya duru zinaripoti kwamba, wakili wa Kabuga alijaribu kuitaka moja ya nchi za Ulaya kumpokea mteja wakem lakini, hata Ufaransa, nchi ambayo alikamatwa mwezi Mei, 2020 baada ya miaka 26 ya kuwa mafichoni haijakubali kumpokea.