Ripoti: Ulanguzi wa dawa za kulevya Afrika Magharibi waambatana na matumizi yasiyodhibitiwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i130846-ripoti_ulanguzi_wa_dawa_za_kulevya_afrika_magharibi_waambatana_na_matumizi_yasiyodhibitiwa
Eneo la Afrika Magharibi linakabiliwa na ulanguzi mkubwa wa dawa za kulevya unaoambatana na matumizi yasiyodhibitika.
(last modified 2025-09-15T23:37:46+00:00 )
Sep 15, 2025 23:37 UTC
  • Ripoti: Ulanguzi wa dawa za kulevya Afrika Magharibi waambatana na matumizi yasiyodhibitiwa

Eneo la Afrika Magharibi linakabiliwa na ulanguzi mkubwa wa dawa za kulevya unaoambatana na matumizi yasiyodhibitika.

Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, eneo la Afrika Magharibi limekuwa eneo la kupitisha dawa zinazozalishwa Amerika Kusini na kusafirishwa barani Ulaya. Licha ya kusafirishwa nchi mbalimbali barani Ulaya, madhara yameanza kujitokeza katika eneo la Afrika MAagharibi. Hali inayozidi kukua.

Mji mkuu Dakar ndio kituo cha matibabu ya uraibu, kitengo pekee cha aina yake katika Afrika Magharibi. Ripoti zinaeleza kuuwa, idadi ya mafaili ya matibabu kutokana na madhara ya madawa ya kulevya imeongezeka mara mbili katika miezi ya hivi karibuni, na kufikia mafaili zaidi ya arobaini kwa mwezi.

Ripoti hiyo inasema kuuwa, nchini Senegal pia mwenendo wa ulanguzi wa madawa ya kulevya umeongezeka sana.

Hivi karibuni tani tatu za mihadharati zilinaswa baharini na jeshi la wanamaji la Senegal. Katika miezi ya hivi karibuni, madawa ya kulevya yalikamatwa kwa wingi hususan kwenye barabara kati ya Dakar na Kidira, nchini Mali, pamoja na Dakar yenyewe.

Kusini zaidi, bandari za Ghuba ya Guinea pia ziko chini ya uangalizi wa karibu. Mnamo mwezi Machi 2024, jeshi la wanamaji la Ufaransa lilinasa tani 10 za kokeini katika maji haya. Kwa ujumla, Afrika Magharibi "iko hatarini sana kupenyezwa na mitandao ya uhalifu, kutokana na eneo lake la kijiografia kuwa katikati ya maeneo ya uzalishaji na matumizi "ngome."