Jenerali wa IRGC: Iran inajitayarisha kujibu vitendo vya uchokozi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139138-jenerali_wa_irgc_iran_inajitayarisha_kujibu_vitendo_vya_uchokozi
Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran laWalinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema vikosi vya ulinzi vya Iran viko tayari kikamilifu kukabiliana na hatua yoyote ya uadui, akionya maadui kwamba nchi hiyo iko tayari kutoa jibu la haraka kwa shambulio lolote.
(last modified 2026-06-14T12:07:04+00:00 )
Jun 14, 2026 12:05 UTC
  • Meja Jenerali Yadollah Javani
    Meja Jenerali Yadollah Javani

Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran laWalinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema vikosi vya ulinzi vya Iran viko tayari kikamilifu kukabiliana na hatua yoyote ya uadui, akionya maadui kwamba nchi hiyo iko tayari kutoa jibu la haraka kwa shambulio lolote.

Meja Jenerali Yadollah Javani, Naibu Kamanda wa IRGC anayeshughulikia masuala ya kisiasa, alitoa kauli hiyo wakati wa hafla iliyofanyika katika wilaya ya Qaen, mkoani South Khorasan, siku ya Jumamosi. Kauli hiyo imetolewa wakati Tehran na Washington zikisema ziko karibu kufikia makubaliano yatakayomaliza kabisa kile kinachoelezwa kuwa uchokozi haramu wa Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Amesisitiza kwa, vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu viko tayari kujibu kitendo chochote cha uchokozi.

Ameongeza kuwa Marekani, Ulaya na nchi za eneo la Asia Magharibi zinapaswa kutambua kwamba Lango-Bahari la Hormuz pamoja na Ghuba ya Uajemi vitasimamiwa kwa utaratibu na mamlaka ya Iran, akisema zama za uwepo wa ajinabi na wanaonyonya rasilimali za eneo hilo zimefikia kikomo.

Amebaini kuwa Marekani na utawala wa Israel zlifanya shambulio lao la kwanza la kijeshi dhidi ya Iran lililodumu kwa siku 12 mwezi Juni 2025. Uvamizi wa pili ulianza mwishoni mwa Februari na kusitishwa mapema Aprili baada ya siku 40.

Amesema katika vita hivyo viwili, mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran pamoja na usimamizi wake imara katika Lango Bahari la Hormuz ni mambo ambayo yaliwalazimisha maadui kukubali usitishaji wa mapigano.

Amesema maadui walianzisha vita wakidhani Iran ingesalimu amri ndani ya wiki moja kutokana na misukosuko ya ndani na shughuli za makundi ya wapinzani wa mapinduzi. Hata hivyo, amesema walikumbana jibu kali la Iran katika medani ya vita  na kulazimika kuomba kusitishwa kwa vita.

Amesema pia wachambuzi wengi wanakiri kwamba Jamhuri ya Kiislamu haikudhoofika, bali imeibuka na nguvu zaidi baada ya vita hivyo na sasa imegeuka kuwa moja ya nguvu kuu nne duniani.