-
Takriban watu 11 wameuawa na 65 kujeruhiwa katika milipuko 2 kwenye maandamano ya M23 huko Bukavu
Feb 28, 2025 04:04Mabomu mawili yalilipuka siku ya jana Alhamisi kwenye maandamano ya waasi wa M23 huko Bukavu, mji uliotekwa na makundi yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuua takriban watu 11 na kujeruhi 65.
-
Mkuu wa haki za binadamu wa UN atadhaharisha juu ya hali mbaya ya mgogoro nchini Sudan
Feb 28, 2025 04:02Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi aligusia mzozo unaozidi kuongezeka nchini Sudan na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa ili kuzuia ukatili zaidi, njaa na watu wengi kuhama makazi yao.
-
ICC yaunga mkono kuundwa mahakama maalum kuchunguza uhalifu DRC
Feb 27, 2025 23:14Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetangaza kuunga mkono kuundwa mahakama maalumu ya kuchunguza uhalifu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Rais Ramaphosa: Mivutano ya kisiasa inakwamisha maendeleo
Feb 27, 2025 23:13Rais Cyrill Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa, mivutano ya kisiasa inatishia maendeleo ya dunia na kwamba ulimwengu utaendelea kurudi nyuma kutokana na kukosekana uthabiti na ushirikiano wa kimataifa.
-
Mgogoro mashariki mwa DRC waathiri zaidi ya wanafunzi milioni 1
Feb 27, 2025 07:32Kuongezeka kwa mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo waasi wa M23 wameshadidisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali, kumesababisha shule 2,594 kufungwa.
-
Misri yapinga pendekezo la Israel la kutaka Gaza isimamiwe na Cairo
Feb 27, 2025 07:31Misri imepinga pendekezo lililotolewa na kiongozi wa upinzani wa Israel, Yair Lapid kwamba Cairo, badala ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas, iendeshe na kuusimamia kwa muda Ukanda wa Gaza; na kusisitiza kuwa mipango ya aina hiyo "haikubaliki."
-
Wasomali 4.4 wanaweza kukabiliwa na njaa kufikia Aprili 2025
Feb 27, 2025 04:31Serikali ya Somalia na mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yalionya Jumatano kuwa watu milioni 4.4 wanaweza kukabiliwa na njaa kufikia Aprili 2025 kutokana na ukame unaozidi, mizozo na ongezeko la bei za chakula katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Ugonjwa usiojulikana waua makumi nchini DRC
Feb 27, 2025 04:24Watu wasiopungua 53 wamefariki kutokana na ugonjwa usiojulikana katika wiki za hivi karibuni katika sehemu ya kaskazini-magharibi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Bunge la Algeria lakata uhusiano na Seneti ya Ufaransa kutokana na Sahara Magharibi
Feb 27, 2025 04:20Baraza la Taifa la Algeria, ambalo ni baraza la juu la bunge, lilisitisha uhusiano wake na Seneti ya Ufaransa siku ya Jumatano kufuatia ziara ya spika wa seneti hiyo katika eneo la Sahara Magharibi linalozozaniwa.
-
Waislamu wa Ghana wamuenzi na kumuomboleza Sayyid Hassan Nasrullah
Feb 26, 2025 23:47Jumuiya ya Waislamu wa Ghana mjini Accra imefanya hafla ya kumbukumbu ya Sayyed Hassan Nasrallah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, ambaye walimtukuza kama shahidi wa Uislamu na ubinadamu.